Kusoma Biblia kila siku sio jambo rahisi sana, au sio jambo gumu sana, au jepesi sana, ila ukiamua kujiwekea ratiba yako kila siku inawezekana kabisa ukasoma Biblia kila siku.

Kuelewa kile unasoma kwenye Biblia sio jambo jepesi sana kwa kila mtu, ila ukiomba Mungu na ukiwa na Roho Mtakatifu ndani yako atakusaidia kuelewa kile unasoma kwenye Biblia yako.

Kujisikia vizuri, au kufili vizuri wakati unasoma Biblia yako sio jambo ambalo linaweza kuwa kwa kila mtu, unahitaji sana kumwomba Mungu akusaidie katika hilo.

Wengi huwa tunaanza kwa kasi sana kusoma neno la Mungu, ila baada ya muda mfupi huwa tunaacha kabisa kusoma neno la Mungu. Hii hali wengi huwa inawaumiza, na huenda umewahi kukutwa na hiyo hali, au unaipitia sasa hivi baada ya kuacha kusoma neno la Mungu.

Narudia tena kusoma neno la Mungu kila siku sio jambo jepesi sana, wala sio jambo gumu sana ila inawezekana kabisa ukasoma Biblia yako kila siku.

Huenda unafikiri haiwezekani kabisa maana umewahi kujaribu Mara nyingi na umeshindwa, ila pamoja na kutoamini kwako, nakuhakikishia unaweza ukaanza tena na ukaweza na ikawa tabia yako ya kila siku.

Nini unachopaswa kufanya? Swali zuri, cha kufanya ni kuamua kwa vitendo, baada ya kuamua ungana na marafiki unaosoma Biblia kila siku na kushirikishana tafakari zao.

Labda unajiuliza hao marafiki utawapata wapi, labda unajiuliza utakuwa unakutana nao muda gani na wewe kazi zako zinakubana sana.

Ondoa hofu, bila shaka simu/laptop unayo ndio maana umeweza kusoma ujumbe huu, una kifaa cha muhimu sana, na kingine hakikisha una Apu ya wasap cha kufanya ni kuwasiliana nasi kwa wasap namba hii +255759808081.

Hiyo namba ichukue na uisevu “chapeo ya wokovu”, alafu nitumie ujumbe wako wasap. Kwanini wasap na utawezaje kusoma neno la Mungu kila siku? Swali zuri, wasap ni jukwaa la kukutana pamoja na kukumbushana kila siku.

Tena kuna namna ya kukufanya ukumbuke kusoma Biblia yako, kwa sababu unawekewa sura ya kusoma kwa siku hiyo. Huwezi kusema huna Biblia wakati huo, unawekewa sura ya kitabu kwenye group la chapeo ya wokovu kwa muda uliopangwa.

Unasubiri nini kuungana na wenzako? Chukua hatua ya kuwasiliana nasi kwa namba +255759808081, utaunganishwa kwenye group hili. Hili group ni la kikristo, haliangalii wewe ni dhehebu gani, linaangalia wewe ni ukristo?

Labda unajiuliza baada ya kukumbuka makundi mengi ambayo umewahi kujiunga, yamekuwa ni makundi ambayo hayaendi na kile yanasema. Kundi hili la chapeo ya wokovu halipo hivyo, kama nilivyokuambia tunaenda vile nimesema hapa kwa msaada wa Mungu.

Soma neno la Mungu ukue kiroho, na chapeo ya wokovu ni jibu lako, ni kundi lenye watu wa rika tofauti tofauti, yaani namaanisha vijana na wazee wapo pamoja katika kusoma neno la Mungu. Kama ulikuwa na hofu juu ya nidhamu ya group, ondoa shaka juu ya hilo.

Kusoma Biblia yako kila siku inawezekana, acha kusubiri siku za Jpili, tena unasubiri uambiwe fungua sura/mstari fulani! Utaishi maisha ya hivyo hadi lini? Usikubali, chukua hatua sasa kwa kuwasiliana nasi kwa wasap namba hii +255759808081.

Mungu akubariki sana.