Chapeo Ya Wokovu – Chapeo Ya Wokovu

About Chapeo Ya Wokovu

This author has not yet filled in any details.
So far Chapeo Ya Wokovu has created 1013 blog entries.

Kazi Nyeti Ya Roho Mtakatifu Anayoitenda Kwa Mwamini

"Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari", Yn 16:14 SUV. Roho Mtakatifu huchukua kile kilicho cha Kristo na kukifunua kwa muamini, kile ambacho kingemletea ugumu kukifahamu yeye anamsaidia kukielewa vyema kama kilivyokusudiwa. Wengi hufikiri ujuzi na ufunuo wa jambo wanapopata watu ni kwa sababu wao wana bahati sana au wana [...]

By | October 1st, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Jambo Lisiloepukika Kwa Mwamini Wa Kweli

"Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu", Yn 15:20 SUV. Iwe makusudi au isiwe makusudi jambo hili huwezi kulikwepa ukiwa mwamini, unaweza kujitahidi kutenda mema ila utakutana nalo. Kuudhiwa itakuwa sehemu yako, kukataliwa, kuchukiwa, kutengwa, kuteswa, kuchekwa, na mengine mengi [...]

By | September 30th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Ujue Uwezo Mkubwa Wa Msaidizi Wetu Tuliyepewa Na Bwana

"Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu", Yn 14:16‭-‬17 SUV. Yesu anamwita Roho Mtakatifu msaidizi wetu, ukiliangalia neno hili "Msaidizi" katika tafsiri ya lugha ya Kiyuyani ni [...]

By | September 29th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Yesu Kuwatawadha Wanafunzi Wake Miguu

"Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga", Yn 13:5 SUV. Kitendo hiki cha kuvutia cha Yesu kuwatawadha wanafunzi wake miguu kilitokea usiku wa mwisho wa maisha yake hapa duniani. Yesu alifanya jambo hili kwa madhumuni yafuatayo; Moja, kuwaonyesha wanafunzi wake ni kwa jinsi gani aliwapenda wao. Pili, [...]

By | September 28th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Je, Mwanaume Kulia Machozi Ni Vibaya?

Sio ajabu kuliona hili hasa kwenye jamii zetu za Kitanzania, mwanaume kulia machozi anaonekana kwenye jamii kama mtu wa kulialia hovyo na asiye na ukomavu wa mambo. Kasumba hii imesababisha wanaume wengi kukaa na uchungu mwingi vifuani mwao huku wakijizuia kulia juu ya mambo yanayowasibu katika maisha yao. Hili halijatokea tu, tangu mtu akiwa mtoto [...]

By | September 26th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Wakati Wa Kupoteza Watu Waliokuwa Pamoja Na Wewe

"Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena", Yn 6:66 SUV. Yesu akiwa anajifafanua yeye ni nani, miongoni mwa watu waliomkimbia au kujiweka pembeni ni wanafunzi wake aliokuwa nao. Ukaribu wa wanafunzi wake inaonyesha wazi bado walikuwa na maswali au mashaka yaliyokuwa yanawakabili. Yesu alipojiweka wazi baadhi yao walirudi [...]

By | September 20th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Miaka Thelathini Na Nane Ya Mateso Magumu

"Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane", Yn 5:5 SUV. Mtu huyu anayezungumzwa na biblia katika andiko hili, alipitia kipindi kirefu sana cha mateso. Kipindi ambacho kilijaa kukata tamaa baada ya kutafuta msaada wa Mungu kwa muda mrefu pasipo mafanikio. Aliendelea kumtumaini Mungu kwa kuamini atamponya na shida [...]

By | September 19th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Upendo Wa Mungu Kwa Ulimwengu Mzima

"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele", Yn 3:16 SUV. Andiko hili takatifu la biblia linatufunua wazi moyo na kusudi la Mungu juu ya ulimwengu huu. Upendo wa Mungu ni mpana kiasi cha kutosha kuwakumbatia watu wote, yaani ulimwengu huu, [...]

By | September 16th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

DIVAI ALIYOITENGENEZA YESU KWENYE HARUSI YA KANA KWELI ILIKUWA NI POMBE?

"Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai", Yn 2:2‭-‬3 SUV. Ukifuatilia aina mbalimbali za Divai utaona zimegawanyika makundi kadhaa yenye kilevi na isiyokuwa na kilevi, lakini tuone Divai aliyotengeneza Yesu. Ipo mitazimo mengi juu ya hili na wapo watu wanaamini divai iliyotolewa mwanzoni mwa harusi [...]

By | September 15th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Ombea Ufahamu Wako Au Wa Wengine Waweze Kuelewa Maandiko

"Ndipo akafungua fahamu zao ili waweze kuyaelewa Maandiko", Luka 24:45 NEN. Tunaweza tusione ladha ya neno la Mungu ilivyo sawasawa, tukasoma na tusione msisimko wowote wa mguso ndani yetu, kutokana na kusoma kama habari zingine kwenye vitabu vingine. Tunaweza kuwalaumu watu hawaelewi kile tunakifundisha au tunakihubiri tukifikiri wanafanya makusudi kutokuelewa yale tunawaambia. Moja ya hitaji [...]

By | September 13th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Watch Dragon ball super