SOMA NENO UKUE KIROHO 637; Kubali Kuonywa Au Kurekebishwa Pale Unapokosea.
Shida ambayo inawatesa watu wengi waliomwamini Yesu Kristo, na kuwa ndani ya wokovu kwa muda fulani, wengi huwa hawakubali kuonywa kuhusu yale wanayoyatenda yasiyompendeza Mungu. Mtu mwingine akionywa au ukimrekebisha kuhusu mwenendo wake mbaya, anaona kama vile umemfanyia jambo lisilo sahihi kwake. Ama mwingine anaweza kuona hustahili kumweleza ukweli kutokana na anavyokuona ulivyo. Tukiwa kama [...]