FIKIRI 31; KINACHOKUFANYA USIJIAMINI.
Kitu kinapozidi kuwa changamoto kwako, inabidi ukae chini na ujiulize nini inakupelekea kuwa hivyo. Hii itakusaidia kurekebisha pale unapoona ndio chanzo ya yote. Ikiwa kwako changamoto kubwa ni kutojiamini, unapaswa kukaa chini na kufikiri nini huwa inakufanya usijiamini. Labda hujiamini kusimama mbele za watu, labda hujiamini kuongea mbele za watu kuwaeleza kile ambacho unatamani wakisikie [...]