Soma Biblia – Chapeo Ya Wokovu

Mambo 5 Unayopaswa Kuyafahamu Kama Unataka Kusoma Na Kutafakari Biblia Yako Kila Siku

Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu, Mungu ametupa neema ya kuweza kuona siku nyingine tena, kuanza wiki mpya kabisa, huu ni upendeleo wa hali ya juu sana kwetu, na tunapaswa kuona ni fursa kwetu kuendelea kulitukuza jina la Yesu. Tunapoanza wiki hii, nikukumbushe safari yetu ya usomaji wa neno la Mungu, moja ya safari ambayo [...]

By | July 10th, 2023|Soma Biblia|0 Comments

Kusoma Biblia kila siku sio jambo rahisi sana, au sio jambo gumu sana, au jepesi sana, ila ukiamua kujiwekea ratiba yako kila siku inawezekana kabisa ukasoma Biblia kila siku. Kuelewa kile unasoma kwenye Biblia sio jambo jepesi sana kwa kila mtu, ila ukiomba Mungu na ukiwa na Roho Mtakatifu ndani yako atakusaidia kuelewa kile unasoma [...]

By | June 26th, 2020|Soma Biblia|0 Comments

SOMA NENO UKUE KIROHO 705; Kitu Gani Ni Ukumbusho Kwako Kwa Bwana?

Maisha ya hapa duniani unaweza ukachagua mwenyewe unataka yaweje kwako, kwanini unaweza kuchagua. Kwa sababu Mungu amekupa uhuru wa kuchagua kuishi maisha ukiwa na Kristo au uamue kuishi bila Kristo. Hata wahubiri wanaohubiri habari njema za Kristo, hamlazimishi mtu kuokoka, mtu mwenyewe anaokoka kwa hiari ya moyo wake. Vile vile mtu akiwa hapa duniani anaweza [...]

By | January 4th, 2020|Soma Biblia|0 Comments

SOMA NENO UKUE KIROHO 704; Unawezaje Kumtambua Mtu?

teachingbibleDownload Mtu anaweza akawa na maneno mazuri sana, maneno ambayo ni matamu sana, maneno ambayo yana ushawishi mkubwa, maneno ambayo anayesikiliza anatamani kuendelea kusikiliza zaidi. Mtu mwingine anaweza akawa na mipango mizuri sana ya mdomoni, mwingine anaweza akawa na ahadi nzuri sana kwa watu. Mtu mwingine anaweza akawa ni mwema kwa maneno yake, vile anazungumza [...]

By | January 3rd, 2020|Soma Biblia|0 Comments

SOMA NENO UKUE KIROHO 703; Ondoa Vile Vitu Vitakavyokuvuta Nyuma Unajikuta Mwaka Unaisha Hujafanya Ulichopanga.

Tupo mwanzoni kabisa mwa mwaka 2020, mwaka ambao tumefika kwa neema ya Mungu. Wapo ambao walikuwa hawana matumaini ya kuufikia ila kwa neema ya Mungu wamefika. Inawezekana hapo ulipo umeshajiwekea malengo yako makubwa ndani ya mwaka huu uwe umeshayafikia, ama baada ya miaka mitano ijayo uwe umeshayafikia malengo yako. Hili Jambo la kupanga malengo yako [...]

By | January 2nd, 2020|Soma Biblia|0 Comments

SOMA NENO UKUE KIROHO 702; Mtu anaweza Kukuambia Uongo Ila Mungu Hawezi.

Hili tumeliona sana kwenye maisha yetu ya kila siku, mtu anakwambia atakufanyia jambo fulani. Lakini anakuja kushindwa kukufanyia kama alivyokuahidi. Mtu huyu aliyekuahidi anaweza akawa aliongea tu kuepuka usumbufu aliokuwa anapata kwa aliyemwahidi atamfanyia jambo au kitu fulani. Lakini aliyeahidiwa anakuja kuona hakutendewa vile aliahidiwa, hajui kuwa kilichomfanya ahaidiwe ni ule usumbufu wake. Wapo watu [...]

By | December 18th, 2019|Soma Biblia|0 Comments

SOMA NENO UKUE KIROHO 701; Wafundishe Namna Watakavyosema.

Kuna maeneo fulani tunakuwa wenyeji wa muda mrefu, tunakuwa tunaelewa taratibu zinavyoenda, tofauti kabisa na mtu ambaye ni mgeni. Kama sio wenyeji tunakuwa tuna uzoefu nayo hayo maeneo au hiyo sehemu, uzoefu ambao watu wengine wanakuwa hawana kabisa. Lakini sisi tunakuwa nao. Sasa wewe kama mgeni ni vizuri kusikiliza utaratibu wa mahali hapo pa ugeni [...]

By | August 29th, 2019|Soma Biblia|0 Comments

SOMA NENO UKUE KIROHO 700; Je, Uliondokaje Nyumbani Kwenu?

Siku unaondoka nyumbani kwenu kwenda kutafuta maisha, uliondoka kwa furaha au kwa huzuni? Siku unaondoka nyumbani kwenu uliondoka kwa hiari yako au ilikubidi uondoke kwa kulazimishwa na ndugu zako au wazazi wako. Uliondokaje nyumbani kwenu, hilo ndio somo letu la leo, somo linalotufanya tufikiri tulipotoka huko na tulipo sasa. Kwanini nimeanza kuuliza swali la uliondokaje [...]

By | August 28th, 2019|Soma Biblia|0 Comments

SOMA NENO UKUE KIROHO 699; Ipo Siku Inakuja Ya Kusahaulishwa Taabu Zako Zote.

Zipo nyakati tunaweza kupita pagumu sana, nyakati ambazo zinakuwa ngumu hata kumwelezea mtu. Na kama unaweza kumwelezea anakuwa hana msaada sana kwako. Wakati tunapitia nyakati kama hizo, mara nyingi huwa tunabaki na upweke fulani hivi wa kukosa usingizi, ama wa kukosa watu wa kuwa nao karibu. Tunapobaki wenyewe, tunakuwa na Mungu pekee, muda mwingine tunaweza [...]

By | August 23rd, 2019|Soma Biblia|0 Comments

SOMA NENO UKUE KIROHO 698; Madhara Ya Mzazi Kumpenda Mtoto Mmoja Kuliko Watoto Wake Wengine.

Tukiwa kama wazazi tuliopata neema ya kupata watoto wa kuwazaa, tunapaswa kuwa makini sana katika hili la kuonyesha upendo wa wazi kwa mtoto mmoja. Bila kufanya hivyo tunaweza kujikuta tumesababisha madhara makubwa kwa mtoto ambaye tunaonyesha upendo wa wazi kwake. Unapaswa kuelewa kuwa upendo kwa mtoto au watoto wako sio mbaya, isipokuwa unaweza kuleta shida [...]

By | August 20th, 2019|Soma Biblia|0 Comments

Watch Dragon ball super