SOMA NENO UKUE KIROHO 686; Usichukue Maamzi Ya Haraka Na Yasiyofaa Baada Ya Majibu Ya Maombi Yako Kuchelewa Kujibiwa.
Yapo mambo tunamwomba Mungu wetu na anajibu kwa wakati, na zipo ahadi za Mungu ambazo ametuahidia katika maisha yetu nazo tunaziona zikitimia kwa wakati wake, na tunaziona na kuzifurahia sana. Yapo mambo mengine tunamwomba Mungu lakini majibu yake bado hatujayapokea, siku za mwanzo tulikuwa na moyo wa subira na kuona Mungu atatujibu tu kwa wakati [...]