“Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai”, Yn 2:2‭-‬3 SUV.

Ukifuatilia aina mbalimbali za Divai utaona zimegawanyika makundi kadhaa yenye kilevi na isiyokuwa na kilevi, lakini tuone Divai aliyotengeneza Yesu.

Ipo mitazimo mengi juu ya hili na wapo watu wanaamini divai iliyotolewa mwanzoni mwa harusi ya Kana na aliyokuja kutengeneza Yesu zilikuwa ni kileo kilichonywewa kwa wingi.

Kama hoja hii inaungwa mkono na wengi au wachache, basi hoja zifuatazo lazima zitambuliwe na kuzingatiwa na wanaoamini hili;

  1. Inawezekana wageni pale kwenye harusi ya Kana wangekuwa wamelewa.
  2. Mariamu, mama yake Yesu, angekuwa anasikitika kwamba kileo kimeisha na angekuwa amemwomba Yesu kuwaongezea wageni ambao tayari wamelewa na divai nyingine yenye kulewesha.
  3. Ili kutimiza matakwa ya mama yake, Yesu angekuwa anatengeneza galoni 120 hadi 180 za divai inayolewesha zaidi (Yn 2:6-9), ambayo ingetosha kuwalewesha wageni waliohudhuria sherehe hiyo.
  4. Yesu angelikuwa anatengeneza divai hii yenye kuelewesha kwa mara ya kwanza kama “ishara ya muujiza wake” ili “kufunua utukufu wake” (Yn 2:11) na kuwashawishi watu kumwamini yeye kama Mwana wa Mungu Mtakatifu na mwenye haki.

Hoja hizi nne nilizotoa hapo juu zenye hoja inayozungumziwa haziwezi kuepukika kwa namna yeyote.

Kudai kuwa Yesu alitengeneza na kutumia divai yenye kileo au kilevi si tu kwamba ni zaidi ya mahitaji ya ufasiri wa maandiko, bali inatupeleka kwenye migongano na kanuni za maadili zilizomo katika ushuhuda mzima wa Maandiko Mtakatifu.

Ni dhahiri kwamba ukizingatia asili ya Mungu, haki ya Kristo, kujishughulisha kwake kwa upendo na wanadamu, na sifa njema ya Mariamu, mawazo hayo hapo juu ya mtazamo kwamba divai pale Kana ilikuwa ya kulewesha ni kufuru.

Tafsiri inayohusisha madai na ukinzani kama huo haiwezi kufuatwa. Maelezo yanayoweza tu kubadilika ni kuwa divai iliyotengenezwa na Yesu kuudhihirisha utukufu na uweza wake ilikuwa ni “juisi za zabibu isiyokuwa na kileo au kilevi”.

Zaidi ya hayo, uwezekano mkubwa ni kwamba ile divai iliyotolewa mwanzo na mkuu wa meza nayo haikuwa na kileo au kilevi.

Kwahiyo, ileweke hivyo kuwa kile kilichofanyika kwenye harusi ya Kana haikuwa pombe, bali ilikuwa divai isiyo na kilevi.

Soma neno ukue kiroho
Kwetu kusoma Biblia ni maisha
Mungu akubariki sana
Samson Ernest