Kitu ambacho tunaweza tusikijue sana katika maisha yetu ni kwamba wapo watu wanapata ujasiri wa kuongea yale mambo magumu kwetu, kwa sababu ipo nguvu ambayo ipo nyuma yao inayowafanya hivyo.

Unaweza ukaumiza kichwa sana na kujiuliza huyu mtoto amepata wapi ujasiri wa kuja kuniambia haya maneno. Kumbe yupo aliye na nguvu nyuma yake, anayemfanya apate ujasiri wa kusema na wewe.

Kwa kuwa hujui unaweza kuanza kupambana na mtoto, bila kujua unajiingiza kwenye mapambano na mtu ambaye amekuzidi uwezo wa kupambana.

Sio kila kitu unapaswa kuparamia, kufanya hivyo utakuwa unapigana vita na watu usiowajua na wakawa wanakujeruhi vibaya sana.

Vizuri kukaa chini na kujiuliza huyo anayekuletea fujo, huyo anayekuja kuongea maneno ya hovyo kwako, huo ujasiri ameupata wapi?

Sio hilo tu, kile ambacho kinapata nguvu kwako unafikiri unachokiona ndio kinasababisha hayo yote? Ukiangalia vizuri utajua sio hicho unachokiona bali ni kingine kabisa.

Pia unaweza ukamwona kijana mdogo anao ujasiri mkubwa ukafikiri anaigiza, kumbe ujasiri alionao ameupata kwa Roho Mtakatifu. Yeye ndiye anayemfanya awe na ujasiri mkubwa alionao.

Mungu akubariki sana.
Samson Ernest.
www.chapeotz.com
+255759808081