
Yesu asifiwe, siku nyingine tena Bwana ametupa nafasi ya kuifikia. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa nafasi hii adimu.
Kifo kinapotamtakwa kwenye masikio yetu, huwa kinatisha na wengi wetu hatupendi kitajwetajwe. Maana huwa tunaona kama mkosi fulani hivi.
Lakini pamoja na kuogopa huko kutajwa kwake, bado haijawahi kutokea kifo kikatoweka katika maisha ya mwanadamu.
Hebu fikiri leo ndio siku yako ya mwisho, kipi kitakuwa alama kwako ya kukumbukwa? Kama unapenda kuandika jumbe mbalimbali za kufundisha wengine.
Ule ujumbe wako wa mwisho utasomeka vipi? Utakuwa ni ujumbe uliojaa mafundisho mema, au utakuwa ni ujumbe tu ambao hueleweki.

Hebu fikiri tu, je unayoyafanya kila siku unapoamka asubuhi yanaweza kukufanya ukaacha alama njema mbele za Mungu hapa duniani?
Wapo watu waliofariki dunia miaka mingi iliyopita ila hatujawasahau hadi leo, hii ni kutokana na matendo yao mema.
Fikiri wewe binafsi kipi kitawafanya watu wakukumbuke, watu wasimame waseme hakika huyu mtu alikuwa hivi na vile.
Watu watoe machozi mengi kutokana na alama njema uliyoiacha hapa duniani, je ni alama gani hiyo ambayo itamfanya kila mtu atoe machozi ya kupoteza mtu muhimu katika maisha yake?
Siku ya leo hili liwe jambo lako la kukufikirisha na kuchukua hatua pale unafanya mambo yako kinyonge. Uamke na kuanza kuishi kwa namna ambayo jina la Bwana litatukuzwe kupitia matendo yako.
Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com
+255759808081