Kabla ya kulalamika jiulize haya;

Je umefanya kazi kama inavyotakiwa?
Je umejituma kama inavyotakiwa?
Je umekaa kwenye nafasi yako inavyotakiwa?
Je umetunza maisha yako ya ujana kama inavyotakiwa?
Je umetunza maisha yako ya wokovu kama inavyotakiwa?

Hebu fikiri tu mwenyewe, kabla hujaanza kulaumu/kuwalalamikia wengine, kabla hujaanza kuwatupia wengine lawama.

Una uhakika umefanya ipasavyo kwa sehemu yako? Una uhakika umekaa vizuri kwenye nafasi yako? Kabla hicho hakijatokea ulisimama vizuri katika eneo  lako?

Fikiri tu utaona kuna maeneo ulipaswa kusimama kwa nafasi yako ila hukufanya hivyo, unachofanya ni kujaribu kuwatupia wengine lawama ili wewe uonekane mwema.

Fanya inavyotakiwa, jitoe inavyotakiwa, dhamiri zako zikushuhudie ndani yako kuwa umefanya kama inavyotakiwa.

Hata kama unamwambia mtu hujafanya vizuri, hata kama unamweleza mtu ukweli, awe anaona unachosema ni kweli.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
www.chapeotz.com