
Watu wengi tunapenda kuona wengine wakitusikiliza kwa makini, wakifanyia kazi yale tunawaambia wayafanye, wakifuata ule ushauri tunawashauri.
Pamoja na kutamani huko bado kuna watu hatupati nafasi hiyo ya kusikilizwa, mtu anaweza akawa anaongea asipewe usikivu wowote na wale anaowalenga.
Achana na ule utulivu wa kulazimisha wengine watulie na kukusikiliza, watu wenyewe wakiwa wanajua una kitu cha kuwaambia wao wenyewe watajenga utulivu wa kutaka kusikia una nini cha kuwaambia.
Kweli unapoanza kuzungumza yale uliyejiandaa nayo, watu wanaokusiliza wanatikisa vichwa vyao kumaanisha kile unasema ni kweli tupu.
Kwa kuwa wengi wetu tunapenda kuona wengine wakitusikiliza kwa umakini mkubwa na kuchukua hatua kwa yale wanapaswa kufanya.
Bado kuna watu wana vitu vizuri vya kuwaambia wengine ila bado wanapuuzwa pale wanaposimama mbele za watu kusema, na kama kwenye radio/tv mtu anabadilisha chaneli.
Watu wanawapuuza kwa sababu wanaona hawana kitu cha kuwaambia, hawana ushauri wa kuwasaidia, kwa kifupi hawana jipya la kuwaeleza/kuwasaidia katika maisha yao.
Pamoja na changamoto hiyo unayopitia sasa ya watu kutokuona umhimu wa kukusikiliza, unafikiri siku wakikusikiliza watakushangaa na kujidharau wao wenyewe kwa kuona una kitu cha pekee ndani yako lakini walikupuuza?
Ndio unaweza ukawa unalalamika watu hawataki kukusikiliza, ama watu wanakudharau, umejipanga kweli kuwapa watu kitu cha kuwasaidia katika maisha yao?
Lazima ufikiri hili, inawezekana kabisa Mungu amekupa kitu kizuri sana cha kuwasaidia wengine. Lakini kama hutajinoa vizuri unaweza ukashindwa kukiwasilisha vizuri hicho kitu Mungu amekupa ndani yako.
Jipange na jiweke vizuri ili siku watu wakikosea kusema ngoja leo tumsikilize tuone ana nini cha kutuambia, iwe ni fimbo kwao ya kuwachapa kwa kukupuuza kwao muda mrefu na waone walichelewa sana.
Kupitia fikiri hii sitamani uwe kwenye kundi la watu watakaoonekana wanawapotezea wengine muda wao. Namaanisha watu watapotenga muda wao kukusikiliza wasione unawapotezea muda wao.
Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
www.chapeotz.com
+255 759 80 80 81