Bwana Yesu asifiwe ndugu, Mungu ni mwema ametupa siku nyingine tena mpya. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu.

Sio kila mahali tunaweza kuwepo, sio kila shutuma tunaweza kusisima na kujitetea wenyewe. Na sio kila shutuma mbaya tunakuwepo wenyewe inapovumishwa juu yetu.

Kwa kuwa hatuwezi kuwepo kila mahali, kwa kuwa hatuwezi kusimama kila mahali kujitetea, na kwa kuwa hatuwezi kuwepo kila mahali inapovumishwa habari mbaya juu yetu.

Unafikiri tabia uliyonayo una uhakika inaweza kumpa mtu anayekufahamu kukutetea au kupinga habari mbaya juu yako? Sio kupinga tu unafikiri anaweza akawa na ujasiri kusema hapo mnasingizia?

Wanaosimama upande wako kukutetea mahali ambapo unashutumiwa kwa kosa fulani, hao wanaokutetea umewatengenezea mazingira ya kusema kwa ujasiri?

Mazingira yako ni tabia yako njema, ikiwa tabia yako mbaya na kinachosemwa ni cha kweli. Uwe na uhakika hata kama watu wako watasimama kukanusha shutuma dhidi yako. Bado ukweli utabaki pale pale kuwa wewe sio mtu salama.

Wakati unaendelea kufikiri wale wanaoweza kusimama na wewe wanaweza kutoa utetezi gani, vizuri sana ukaishi maisha matakatifu. Maisha yanayompendeza Mungu wako.

Hii itakufanya hata wale ambao Mungu anawainua wakutetee mahali ambapo huwezi kutoa utetezi wako. Watu hao wasiambulie aibu, maana kama watakutetea kinyume na uhalisia wako mwisho wao utakuwa ni aibu.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
Blog: www.chapeotz.com
WhatsApp: +255759808081.