“Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena”, Mk 3:5 SUV.

Hapa Hasira ya Yesu inaonesha wazi chuki yake na kutokubaliana na matendo yasiyo ya haki kwa watu, yaani matendo maovu.

Ingawa wakristo tunapaswa kupinga vikali hasira isiyokuwa ya haki, lakini kuwa na hasira dhidi ya maovu yanayotendeka ni kufanana na Yesu Kristo.

“Hata alipoyakaribia marago akaiona ile ndama, na ile michezo. Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima”, Kut 32:19 SUV.

Musa naye anaonyesha wazi vile aliona wana wa Israel wamemwacha Mungu wao na kujitengenezea ndama wa sanamu ambaye walikuwa wanamwabu.

Hasira ya Musa iliwaka ndani yake, Musa ni mfano bora wa mtumishi aliyepewa dhamana ya kulichunga kundi alafu kundi likawa limeiacha njia sahihi.

Ukiwa unaona mambo yanaenda ndivyo sivyo alafu ndani yako una amani na utulivu, hii ni udhihirisho kuwa uhusiano wako na Mungu haupo vizuri.

Mtu aliye na Roho Mtakatifu ndani yake, na aliye na njia safi mbele za Mungu, anapoona mambo yanaenda kinyume na neno la Mungu, hasira ya Kimungu lazima iwake ndani yake.

Hiyo ndio hasira anayopaswa kuwa nayo mwana wa Mungu, nje na hapo tunapaswa kujizuia tusimtende Mungu dhambi.

Tunaweza kukutana na mambo mabaya kwenye maisha yetu, mambo yanayotufanya tupate hasira. Tunapokutana na hali hiyo tunapaswa kujilinda ili tusimtende Mungu dhambi.

Tuonapo mambo yasiyofaa mbele za Mungu, tusiogope kukemea kwa nguvu zote, wala usijali hasira na wivu wa Bwana unapowaka ndani yako.

Soma neno ukue kiroho
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081