Shalom, tunapenda kufahamu kama unapokea jumbe mbalimbali tunazokutumia kila wakati, na kama unapokea kuna kitu gani umejifunza na umekifanyia kazi na kukuzalia matunda katika maisha yako.
Tunapenda kufahamu hili ikiwa kuna kitu unanufaika kupitia makala tunazokutumia kwa njia hii ya email, hata kama unaona ni jambo dogo usisite kutushirikisha hapa kwa kujibu email hii (reply).
Ujumbe utakaotuma hautaonekane sehemu nyingine zaidi ya hapa, utaonwa na admin tu, kwa hiyo uwe huru kutuandikia chochote, iwe ni ushuhuda au vile masomo haya yanakubariki.
Lengo ni kufahamu kama unabarikiwa na masomo tunayokutumia kila mara, na kama una ushauri wowote unaweza kutuandikia kwa kujibu email hii.
Tutafurahi kupokea mrejesho wako.
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081