
“Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu”, Mt 24:42 SUV.
Kesheni ni neno linalosisitiza wakati uliopo au sasa, likionesha kudumu katika kuwa macho na kukesha katika wakati wa sasa.
Sababu ya kukesha wakati huu tulionao sasa, badala ya kusubiri hapo baadaye ni kwa sababu waamini wa sasa hatujui ni wakati gani Bwana atakaporudi kuja kutuchukua au kulichukua kanisa.
“Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo”, Yn 14:3 SUV.
Hapatakuwepo na ishara au tahadhari ya siku au tarehe fulani Yesu atakuja, hii inaweza kuwapelekea wengine kuona Yesu anaweza asirudi leo.
Kwa maneno mengine tunaweza kusema, tunapaswa kuzingatia uwezekano wa kihistoria kuwa Kristo anaweza kurudi wakati wowote.
“Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja”, Mt 24:44 SUV.
Kurudi kwa Yesu Kristo kuja kulichukua kanisa itakuwa siku yeyote, hatuna budi kujiandaa sawasawa.
Atarudi, kama kuna mtu anakuambia Yesu hatarudi tena, huyo atakuwa anakudanganya, kaa ukijua Yesu anarudi wala hatakawia.
Uwe tayari, njia zako ziwe safi, kama sio safi hakikisha unatengeneza njia zako, siku itakapofika uwe tayari kwenda na Bwana.
Mungu atusaidie sana
Samson Ernest