“Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo”, Mt 16:6 SUV.

“Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo”, Mt 16:6 SUV.

Kwanza tufahamu “chachu” ina maana gani, chachu inayozungumzwa hapa ni ishara ya uovu na uharibu, inaelezea hasa kuhusu mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

Yesu anayaita mafundisho yao “chachu” kwa sababu hata kiasi kidogo cha mafundisho kinaweza kupenya na kuathiri kundi kubwa la watu kuamini kitu kisicho sahihi na kilicho kinyume na neno la Mungu.

Akawaagiza, akasema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode”, Mk 8:15 SUV.

Nguvu ya mafundisho ni kubwa sana na inatenda kazi kwa mtu atakayesikiliza na kuamini kile alichosikia, anaweza kuondoa kile kizuri kilichopandwa ndani yake na kuingiza kitu kisicho sahihi katika maisha yake ya wokovu.

Ndio maana leo tunaweza tukawa kwenye imani moja katika Kristo ila mmoja wetu akawa na mtazamo unaopingana na imani yake, mtu kama huyo huwa hana siku nyingi atakuwa ameacha imani ya kweli na kugeukia imani isiyo sahihi au potofu.

Tukiwa watu waliopata neema ya wokovu tunapaswa kuwa makini sana na kujilinda na mafundisho yaliyo kinyume na neno la Mungu, yapo mafundisho yanalitaja jina la Yesu ila ndani yake yamejaa ukengeufu mkubwa.

Siku hizi kuna mafundisho yaliyojaa ungeufu mwingi, na yanasambaa kwa kasi kwa njia ya teknolijia, mwamini usipokuwa makini unaweza kuacha imani ya kweli na kukimbilia imani potofu.

Upande mwingine mafundisho yanayosambazwa kwa njia ya mitandao yanaweza kukutoa gizani na kukuleta nuruni, muhimu ni kujua mafundisho sahihi ni yapi na yasiyo sahihi ni yapi.

Tahadhhari aliyotoa Yesu, hata kwetu tunapaswa kuizingatia, chachu ya Mafarisayo na Masadukayo ipo katika ulimwengu wa sasa, ukikutana nayo na kuiamini uwe na uhakika utakuwa umepanda uovu ndani yako.

Ukiwa imara kwa kujaa neno la Mungu na mafundisho sahihi ya neno, sio rahisi kupandikizwa hii chachu, maana utakuwa unajua fundisho sahihi na lisilo sahihi, changamoto kwa mchanga wa kiroho anaweza kuamini kila neno.

Mjinga huamini kila neno; Bali mwenye busara huangalia sana aendavyo. Mwenye hekima huogopa, akajitenga na uovu; Bali mpumbavu ana ufidhuli, na kujitumai”, Mit 14:15‭-‬16 SUV.

Jilinde sana na chachu, ambayo ni mafundisho potofu yenye nia ya kupotosha njia zako sahihi mbele za Bwana, kwanini imani yako igeuzwe na kupokea imani isiyo sahihi? Usikubali hata kidogo, uwe mwenye hekima.

Nikualike kwenye kundi la wasap la kukufanya ukue kiroho kwa kusoma biblia na kutafakari kila siku, kwa mtiririko mzuri uliowekwa na wote wanaoufuata hufanikiwa, wasiliana nasi kwa wasap +255759808081 ili uwe kuungwa kwenye kundi.

Soma neno ukue kiroho

Mungu akubariki

Samson Ernest