Siku za leo wanaoigiza wanampenda Mungu ni wengi na wale ambao hawaigizi ni wengi.

Wanaoigiza wanaishi maisha ya kumpendeza Kristo ni wengi, na wasioigiza ni wengi pia.

Mtu yeyote anayempenda Yesu na kumaanisha katika Roho na kweli, mtu huyo hawezi kujificha.

Hata kama watakuwepo wasanii wa kuigiza, bado wao watajipagua na kuonekana kwa namna ya pekee kabisa.

Mungu wetu ni mwaminifu sana, ukimtafuta utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote.

Rejea: Lakini huko, kama mkimtafuta BWANA, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote. KUM. 4:29 SUV.

Hili lipo wazi kabisa, bidii yako kwa Mungu ina matunda yake. Hata kama sio leo, uwe na uhakika utavuna ulichopanda.

Kumpata Mungu ni kujitoa haswa bila mchezo, sio hivi hivi lazima ujikane nafasi yako.

Ukifanya hivyo utamwona Mungu kwa viwango vingine mwaka 2020.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.