
“Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?” Mt 7:16 SUV
Walimu au wachungaji au mitume au manabii au wainjilisti wa uongo ambao kwa nje wanaonekana wenye haki lakini kwa “ndani ni mbwa mwitu wakali”.
“Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali”, Mt 7:15 SUV.
Kuna nyakati wanaweza kutambuliwa kirahisi kupitia matunda yao, yale matendo yao yanavyojidhihirisha kwa uwazi yanaonyesha wazi tabia zao za ndani zilivyo.
Tunda la walimu wa uongo, au wachungaji, au manabii, au mitume, au wainjilisti wa uongo litadhihirika kwa sifa mbaya katika maisha ya wafuasi/waumini wao.
“Hao ni wa dunia; kwa hiyo wanena ya dunia na dunia huwasikia Sisi twatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu atusikia; yeye asiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili twamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu”, 1 Yoh 4:5-6 SUV.
Sifa 5 zifuatazo zitaonyesha wazi kwa waumini au wafuasi wao walivyojaa mafundisho ya uongo;
- Watakuwa ni watu wanaokiri kuwa Wakristo ambao utiifu wao au nidhamu yao inakuwa juu zaidi kwa watu mashuhuri hasa walimu au manabii wao kuliko neno la Mungu (Mt 7:21).
Wanakuwa wanamwabudu mtume au nabii au mchungaji wao kuliko Mungu muumba wa mbingu na nchi (Rum. 1:25).
- Watajishughulisha zaidi na tamaa zao wenyewe za mwili kuliko yale mambo yanayompa Mungu sifa na utukufu na heshima.
Mafundisho yao yatalenga zaidi kwenye ubinafsi wa kujinufaisha wao kuliko Mungu, ili wajipatie fedha au mali nyingi kwa manufaa yao wenyewe.
- Watayapokea mafundisho na mapokeo ya kibinadamu hata kama yanapingana na ukweli wa neno la Mungu (Mt 7:24-27).
- Watatafuta na kukubali uzoefu wa kidini na madhihirisho ya miujiza kama mamlaka ya mwisho katika kuhalalisha kweli (Mt 7:22-23), badala ya kujikita katika ushauri wa neno la Mungu.
Kwao miujiza ya uponyaji na matendo mengine ndio ishara nzuri kwao, bila kujua hata Shetani naye ana ishara na miujiza.
- Hawatayastahimili mafundisho ya kweli bali watatafuta walimu watakaowapa wokovu pamoja na barabara pana iliyo kinyume na neno au haki (Mt 7:13-14).
Waumini wao watakuwa tayari kusikia injili laini zinazowalea katika matendo yao maovu, injili ambazo haziwagusi maisha yao ya dhambi.
Watu kama hawa ujue ni matunda ya walimu wa uongo, watu waliomeza mafundisho yaliyo kinyume na neno la Mungu.
Ndugu mpendwa unapaswa kujihadhari sana, mahali ambapo unaona unafanya dhambi alafu unaambiwa sio dhambi ujue upo mahali sio sahihi.
Karibu uungane nasi ujifunze neno la Mungu ukue kiroho, ungana nasi kwa wasap +255759808081, wasiliasiana nasi kwa namba hiyo utaunganishwa kwenye kundi la wasap la kusoma neno la Mungu.
Mungu atusaidie sana
Samson Ernest
+255759808081