Wito kwa wazazi wote katika malezi ya watoto, hili linapaswa kuwa kipaumbele cha kila mzazi mwenye watoto.

Watoto kabla ya kwenda Sunday school, wanapaswa kuwa na mafundisho ya kutosha kutoka wazazi wao.

Sio mafundisho tu, mafundisho ya neno la Mungu. Mafundisho ambayo yanamfanya mtoto awe katika njia impendezayo Mungu.

Zile ibada zetu za pamoja tunapaswa kupanda mafundisho ya neno la Mungu kwa watoto wetu.

Hili ni agizo la kibiblia kabisa, ikiwa ni agizo la kibiblia tunapaswa kujenga msingi imara kwa watoto wetu.

Rejea: nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. KUM. 6:7 SUV.

Mtoto mwenyewe akaharibike huko ila ukiwa kama mzazi, unapaswa kuwekeza maarifa ya kutosha kwa watoto wako.

Mahali popote pale unapokuwa, unapaswa kuwekeza maarifa ya neno la Mungu kwa watoto wako.

Ndio maana tunasisitizana kila mara tusoma neno la Mungu kila siku na kutenga muda wa kutafakari yale uliyojifunza.

Hii inatufanya tuwe imara kwenye eneo la kufundisha watoto wetu maarifa sahihi ya neno la Mungu.

Wazazi tunapaswa kuzingatia sana hili, hasa wale ambao bado watoto wao wanaweza kufundishika. Vizuri sana kuwapandia maarifa ya kuweza kuwasaidia katika maisha yao.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
www.chapeotz.com