
Wengi wetu tunaogopa sana kuhusu kifo, na ukitaka kukosana na baadhi ya watu mweleze kuhusu habari ya kufa, utaona anabadilika au anakukemea uache kumtakia mabaya.
Pamoja na kuogopa kwetu kuhusu kufa, bado watu hawana hofu kutenda dhambi, dhambi zinafanywa waziwazi bila uoga wowote. Na watu wanaona hawana shida kabisa.
Japo duniani huwa tunajaribu kuwapa maneno mazuri na kuyafunika yale mambo yao mabaya, lakini wakati mwingine tukija katika uhalisia utaweza kuona kabisa hakuwa vizuri na Mungu.
Sasa ndugu tunapoishi hapa duniani, tunapaswa kuelewa ipo siku tutaondoka hapa duniani, na baada ya kifo tu ni hukumu mbele za Mungu. Hili linapaswa kukaa kwenye mioyo yetu au vinywa wetu.
Rejea: Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu. EBR. 9:27 SUV.
Ndugu hakuna mambo mengine yataendelea pale utakapoondoka hapa duniani, usifikiri kuna ofa nyingine tena baada ya kifo. Baada ya kifo ni hukumu ndio inafuata.
Chochote unachokifanya hapa duniani uwe na kumbukumbu kuwa ipo siku ya kwenda kusimama mbele za Mungu, hukumu ipo kwa wale ambao hatateswa na jambo lolote.
Mungu atusaidie sana tumemalize mwendo salama.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com