
Upo umhimu mkubwa sana wa kuwakumbuka watumishi wa Mungu waliolihubiri Neno la Mungu hadi tukaokoka, wanaweza wakawa kwenye nafasi zao au wanaweza wakawa hawapo kwenye nafasi zao kutokana na umri wao.
Sio watu wote wataliona hili na kulichukulia kwa uzito mkubwa sana, bali ni wale watu wa Mungu atakaowakusudia waifanye kazi yake. Watakuwa na mzigo ndani yao ila na wao wasipopata maarifa ya kutosha mioyoni mwao wanaweza wasifikie kwenye lengo.
Lakini ukiwa kama mtu unayejifunza neno la Mungu kila siku, huwezi kuwa na sababu ya kujitetea kuhusu hili kuwa hukujua. Kama hukujua leo utakuwa umejua baada ya kujifunza somo hili la leo.
Wakati mwingine wapo wachungaji ambao wamelea washirika kwa miaka mingi sana ila wakati ambao hawana nguvu tena ya kuendelea, washirika hao wanakuwa hawawakumbuki hao wachungaji ambao waliowapa Neno la Mungu.
Jambo lingine la muhimu sana hatupaswi kuishia hapo kutokana na nilivyoeleza hapo juu, tunapaswa kuiga mwenendo wao safi. Lingine kubwa sana ni kuiga imani yao.
Rejea: Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao. EBR. 13:7 SUV.
Hebu tusiwasahau watumishi wa Mungu waliotulea kiroho wanapaswa kutiwa moyo, bila kutafuta muende na nani unaweza kujenga utaratibu huo wa kwenda na zawadi nzuri za kumfanya afurahia matunda ya huduma aliyokuwa anaifanya.
Hasa watumishi wazee, maeneo mengi ya nchi yetu wamewasahaulika sana watumishi hawa wa Mungu, wakati aliokuwa anawafundisha neno la Mungu yupo na wao wapo.
Jali watumishi wa Mungu, wasifike mahali wakaona hawana mtu wa kuwajali na kuwasikiliza pale wanapohitaji msaada fulani uwasaidie. Bila kusahau kujifunza mwenendo wao mzuri wa imani yao.
Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com