Hii ni neema ya ajabu sana, tena ya kushangaza sana kwa jinsi ilivyo na mambo yasiyofikirika kibinadamu kama yanawezekana kutokea kwa mwana wa Mungu.

Upo wakati mtu anakuwa na shida kweli, wakati ambao anakuwa anapitia kwenye wakati mgumu sana katika maisha yake ya kawaida. Ambapo kipindi kama hicho mtu anakuwa kwenye maisha yale yale.

Nyakati kama hizo ngumu kwake hufika wakati anachoka na kuona kila jambo kwake ni baya, na wengine hufikiri mbali zaidi kutaka kujidhuru maisha yao. Hii hutokana na mtu kuvunjika moyo wake, na kupondeka roho yake.

Mtu kama huyu anapokuwa amevunjika moyo wake, sio kana kwamba hakuna msaada wake, msaada wake upo Bwana. Bwana ndiye anayeweza kuwafariji na kuwatia nguvu mpya wale wote waliokosewa.

Rejea: BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa. ZAB. 34:18 SUV.

Mambo tunayokutana nayo ni mengi sana, yapo mambo mengi yanayoumiza mioyo yetu sana, lakini tumeona kuwa anayeweza kuwa Karibu nawe ni Mungu mwenyewe.

Huenda hapo ulipo sasa unapitia hali fulani mbaya ya kuumiza moyo wako, hadi umefika mahali unashindwa kuelewa ufanyaje. Fahamu jambo moja tu, tena kwa imani, kuwa Bwana yupo nawe atakusaidie.

Je umevunjika moyo? Jibu lako lipo kwa Bwana, muhimu sana ni wewe kukubali kukaa vizuri na Mungu wako, huku ukiendelea kuishi maisha yanayompendeza Mungu.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com