Hakuna ubishi wala hupaswi kupindisha ukweli wa mambo, ya kuwa Yesu Kristo alikufa na akafufuka siku ya tatu, kwahiyo tunayemwamini ambaye ni Yesu Kristo tupaswa kukiri hili ili imani yetu iwe sawasawa.

Hapa ndio msingi wa imani yetu ulipo, tuna jivunia hili, maana tunayemwamini alikufa na akafufuka siku ya tatu. Kisha akaenda kuzimu kumnyang’anya shetani funguo.

Kwahiyo mwenye funguo za mauti na za kuzimu ni Yesu mwenyewe, hakuna awaye yote mwenye hizo funguo ni yeye peke yake. Hili linapaswa kufahamika kwako uliyeokoka, wakati usipokuwa na ufahamu wa hili unaweza ukawa unapata shida kutamka mbele za watu.

Hili lipo wazi kabisa na Yesu mwenyewe anakiri wazi kupitia Neno lake kuwa alikufa na sasa yupo hai milele, sijui kama unaelewa maana ya milele. Maana yake haina mwisho, siku zote yeye yupo hai, tena jambo lingine la kufurahisha zaidi, anazo funguo za mauti na za kuzimu.

Rejea: Na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. UFU. 1:18 SUV.

Chunguo lako la kumkubali na kumwamini na kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yako ni sahihi kabisa, maana yeye ni njia ya kweli na uzima. Hakuna mtu yeyote atakayeweza kuingia mbinguni pasipo kupitia njia yake.

Utaona ni jinsi gani imani yetu ipo vizuri, kwa sababu msingi wa imani yetu upo vizuri na unaeleweka kabisa, laiti kama Yesu angekufa moja kwa moja pasipo kufufuka. Tusingekuwa na ujasiri, tena tusingekuwa na mamlaka ya kumkemea shetani.

Furahia wokovu wako, mfurahie Yesu Kristo, furahia imani yako, ulipo ni sahihi, na unayemwamini ni sahihi kabisa, maana yeye ndiye mwenye funguo zote.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com