Tunaweza kufanya mambo makubwa sana na mazuri sana, mambo ambayo yanamtukuza Mungu wetu, mambo ambayo yanaigusa jamii yetu inayotuzunguka kwenye mazingira yetu tunayoishi.

Tunaweza kufanya mambo mabaya sana, mambo yanayoumiza mioyo ya wengine, mambo yanayowafanya wengine wajute kwanini walizaliwa duniani. Wanajiuliza hayo maswali mengi ambayo yanaibua hisia nzito ndani ya mhusika.

Katika hayo mambo, yaani mazuri na mabaya, unapaswa kuelewa kile ulichokuwa wanatendea wengine kiwe kizuri au kibaya. Ujue kitakurudia na wewe, hata kama huoni sana matokeo yake sasa hivi, wewe jua kitakurudia tu.

Rejea: Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu. UFU. 13:10 SUV.

Unaweza ukachukulia ni maneno tu ila nakwambia sivyo hivyo unavyofikiri, chochote ukifanyacho kina mshahara wake, kama ni kizuri kina malipo yake na kama ni kibaya kina malipo yake pia.

Tukiwa kama wakristo tunapaswa kusimama imara haswa, bila kugawanyika makundi makundi ambayo hayampendezi Mungu. Yakimpendeza Mungu ni heri sana kuliko kuwa chukizo mbele za Mungu.

Mungu atusaidie sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
+255759808081