Asifiwe mwokozi wetu Yesu Kristo aliyejitoa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, siku nyingine tena Bwana anaendelea kutupa kibali cha kuiona. Kwa kawaida unaweza kuchukulia ni kawaida kulala na kuamka, ila fahamu sio jambo la kawaida kabisa, wapo watu wamehangaikia afya zao huku na kule ili waendelee kuwa hai, lakini haikuwezekana.
Zoezi la kusoma NENO la MUNGU, bado linaonekana jambo gumu kwa wengi wetu, ugumu huu umeendelea kuletwa na sisi wenyewe kwa kufikiri jinsi tunavyoweza kufikiri wenyewe.
Nimesema sana hii kauli ya huna sababu ya kusingizia hili, ili usisome NENO la MUNGU, kwa ulimwengu wa sasa zipo smartphones, zipo tablets, zipo laptops, hizi zote unaweza kusoma NENO mahali popote ulipo.
Vifaa hivi vyote vinakuwezesha kuwa na biblia ya lugha unayoitaka wewe, labda ukitaka kilugha chako ndio itakuwa tatizo. Ila ukita lugha za kimataifa utazipa kwa njia ya maandishi na sauti.
Zoezi hili linategemea sana NIDHAMU yako, wala halihitaji muujiza mkubwa sana kwako, kinachohitajika ni wewe kuamua kuachana na sababu zisizo na msingi sana kukwamisha kusoma NENO la MUNGU.
Kila mmoja yupo bize, kila mmoja anakutana na changamoto zake ambazo zinamfanya akili yake iwe na mzigo wa kuwaza namna ya kuitatua. Pamoja na hayo yote, hatuwezi kuacha kumpa muda MUNGU.
Mtatuzi wa changamoto zetu ndiye tunahimizana kujifunza habari zake, NENO LAKE ndio lenye maelekezo sahihi ya namna ya sisi kuishi. Kuishi kwako kunategemea sana Mungu, ikiwa ni hivyo iweje hatuoni umhimu wa kutenga muda wetu wa kusoma NENO.
Kweli kabisa zipo changamoto hutukuta ambapo tunashindwa kwa wakati huo kutenga muda wetu kwa ajili ya NENO, ila haiwezi kuwa kila siku wewe ni mtu wa kuendekeza msongo wa mawazo, kukusababisha ushindwe hata kusoma NENO kila siku.
Muhimu sana kujua kwanini unapaswa kuwa msomaji wa NENO, hili halihitaji ujipange, ikiwa umeamua kumpokea YESU Kristo kama Bwana na Mwokozi wako. Lazima ujitoe kulisoma NENO lake, maana linakupa maelekezo ya maisha yako yote.
Utaona kama nakutania hapa, utaona nakushawishi, ila hakuna ukweli, unaweza ukawa upo sawa kutokana na marafiki ulionao. Lakini kujiona kwako upo sawa ndio kumekupoteza na kukufanya uendelee kuwa pale pale. Umeshindwa kushinda dhambi kwa sababu huna neno ndani yako, umeshindwa kuwa na moyo wa msamaha kwa ukosefu wa NENO.
NENO LA MUNGU linakupika kiasi kwamba huwezi kuruhusu chochote kilicho kichafu kiote na kijenge mizizi ndani yako. Utakapogundua ulichofanya ni kibaya mbele za Mungu, itakuwa rahisi sana kwako kujirudi haraka kuliko asiye na NENO.
Asiye na NENO, yeye hujiona yupo sahihi, ukimwambia mbona unapaswa kusamehe hili, atakupa sababu za kutosha za yeye kutoweza kumsamehe kamwe aliyemkosea.
Hakuna kwenye biblia ambapo kunaelekeza makosa ya kusamehe sisi na ambayo hatuwezi kusamehe, haijalishi ulitendewa nini, unapaswa kusamehe na kuachilia moyoni mwako.
Unaweza kuona kama hadithi ila ukiwa na NENO la kutosha ndani yako inawezekana kabisa, mahusiano yako mazuri na Mungu yanategemea sana wewe.
Raha ya kulijua NENO ni kwamba, una uwezo wa kuomba msamaha hata kama wewe hukukosea, huwezi kuwa na kisasi moyoni mwako. Hata kama utavurugwa sana, baada ya muda fulani utapata utulivu moyoni mwako kwa sababu utaanza kupata mafundisho ya akiba uliyonayo moyoni mwako.
Nimejaribu kukupa faida chache za kusoma NENO, eneo hili la kusamehe na kutokuwa na kisasi juu ya mtu, linawatesa wengi wetu. Mtu yupo tayari kutamka maneno kama haya; “atanijua mimi ni nani” ananiona mimi ni wa kuja sio, ataniona mimi huwa siguswi ovyoovyo!
Ukimwangalia ni mkristo safi kabisa, hapo ndipo utajua huyu mtu amebeba dini/dhehebu moyoni, na si Yesu moyoni, na kuliweka NENO la MUNGU moyoni.
Hebu amua LEO kuanza kutulia na biblia yako kwa ajili ya kusoma vitu vya kukujenga kimwili na kiroho, usisubiri malaika ashuke aje akuambie hili, unaweza usimwone kabisa, ndio maana Mungu anatumia watu wake kukufikishia hili.
Umeshaanza mpango huu wa kujisomea NENO la MUNGU, ila unajiona kuna vitu bado hujaviweka sawa, jitahidi sana kuviweka sawa ili uendelee kuwa mwanafunzi mzuri wa YESU. Unapaswa kuwa msikiaji wa neno na mtendaji wa neno, unapaswa kuwa msomaji wa neno na mshikaji wa neno, na kuyatenda yale unayosoma/kujifunza.
Leo tupo katika kitabu cha 1 Nyakati 21, kwa wale ambao tupo wasap group, tunaenda kusoma na kushirikishana yale tuliyojifunza katika sura hii. Unapenda kuwepo na wewe katika group hili, na umedhamiria kutoka ndani ya moyo wako, unakaribishwa sana kwa kuwasiliana nasi kwa namba hizo chini.
Mungu afungue moyo wako upate kuelewa zaidi umhimu wa kusoma NENO Lake.
Samson Ernest.
+255759808081.