Nakusalimu katika katika jina la Yesu Kristo aliye hai sasa na hata milele. Siku nyingine tena Bwana amtupa ili tuendelee kuitenda kazi yake na kujirudi pale tulipomkosea.

Tunaendelea kujifunza NENO la MUNGU kwa njia ya kusoma biblia, hatua hii imekuwa njema na imeendelea kuzalisha watu waliokomaa KIROHO.

Kila aliye maanisha kusoma NENO na kupata muda wa kutafakari, ipo hatua kubwa amesogea KIROHO.

Huenda uliona hili jambo haliwezekani kutendeka, nikuambie kwamba kusoma biblia inawezekana kabisa katika maisha yako yote ya wokovu.

Mtu anayejua NENO vizuri hasumbuliwi na jambo lolote, yote yanayotokea chini ya jua, yalishaandikwa na tumepewa njia ya kufuata pale tunapojikuta tupo wakati mgumu.

Nakusihi sana sana endelea kutenga muda wako wa kujifunza NENO la MUNGU, haijalishi unakutana na changamoto gani. Tengeneza utaratibu ambao utakuwa tabia yako ya kujifunza maisha yako yote.

Unajiuliza utaratibu upi huo, ni kama ulivyojiwekea muda wa kunywa chai, na muda wa kula chakula cha mchana na jioni. Vile vile ulivyojiwekea utaratibu wa kulala na kuamka, ndivyo unavyoweza kujiwekea utaratibu wa kusoma NENO la MUNGU.

Ipo nguvu ipatikanayo ndani ya NENO la Mungu, ikiwa ni hivyo lazima adui akuwekee vikwazo vya kushindwa kuwasiliana na Baba yako aliye mbinguni, kataa hilo la kukwamishwa.

Leo tunaenda kujifunza NENO katika kitabu cha 1 Nyakati 10, nikukaribishe sana tupate kujifunza kwa pamoja.

Unapenda kuungana nasi katika kujifunza NENO la MUNGU, tuma ujumbe wako whatsApp wenye majina yako kamili kwa namba hizo chini.

Endelea kutembelea mtandao wetu wa Chapeo Ya Wokovu kwa masoma mazuri zaidi.

Samson Ernest.

+255759808081.