Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo aliye hai, habari za leo ndugu katika Kristo, bila shaka umeamka vyema na umeendelea kupambana na mambo yanayokuhusu siku ya leo.
Kujifunza ni kila siku ukiwa umechagua kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo, hakuna siku utahitimu na kujiona uhitaji tena chochote cha kujifunza.
Mwanafunzi anahitajika kuwa mtu wa kusogeza hatua fulani tofauti na jana, utofauti huu unaletwa na bidii yake binafsi pale anapojitoa kila wakati kujifunza.
Tunasema hakuna kuhitimu mambo ya KIROHO kwa sababu tunahitaji shibe ya kiroho kila leo, haijalishi umekuwa mzee bado unamhitaji Mungu akusaidie zaidi ili umalize safari yako salama.
Pasipo bidii tutajikuta tunaishia njiani na adui anapata nafasi ya kutupiga, maana uwepo wa MUNGU unakuwa haupo pamoja nasi.
Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu, nguvu zinazozungumzwa sio za ugali, bali ni wale wenye bidii ya kuutafuta uso wa Mungu.
Leo tupo kitabu cha 1 Nyakati 11, nakusihi sana utenge muda wako wa kusoma NENO na kutafakari kile umejifunza.
Unaweza kuona biblia ni kitabu kisicho na story tamu kama ulivyozoea kwenye vitabu vingine, fahamu kwamba NENO la MUNGU, ni Mungu mwenyewe adui anajua hilo ndio maana anakuwekea uzio ili uone mateso kujisomea NENO.
Amua leo kujitoa kwa kila hali, ruhusu Roho Mtakatifu akuongoze katika hili, pamoja na unapaswa kujitoa wewe kama wewe. Ila hakikisha unajiunganisha na nguvu ya Roho Mtakatifu ili upate kuelewa kile Mungu amekikusudia ukielewa kwenye NENO lake.
Nikualike wewe ambaye ulikuwa bado hujaanza kusoma NENO, anza leo kusoma, usisubiri kesho ndio useme utaanza, anza sasa.
Unaona huwezi kujisimamia mwenyewe na una simu yenye uwezo wa WASAP, ondoa shaka unaweza ungana nasi kwa mawasiliano +255759808081. Hakikisha umeokoka na una nia ya kusoma NENO, na hakikisha unatuma jina lako kamili kwenye namba hizo.
Mungu akubariki sana wewe uliyejua umhimu wa kujifunza NENO, tamani na mwenzako ajue jambo hili. Ombea wengine na wao wasikie kiu ndani yao ya kujifunza NENO la MUNGU.
Usiache kutembelea mtandao wetu wa Chapeo Ya Wokovu kwa masomo mazuri zaidi ya NENO la MUNGU.
Nakutakia wakati mwema.
Samson Ernest.
+255759808081.