Kuna tofauti kati ya kupendwa na kuchaguliwa, kuna watu wengi walipendwa lakini wewe ukachaguliwa kuwa mume/mke wa huyo mtu, kumbuka pia kuna wenzako waliwahi kupendwa, lakini katika kuchaguliwa hawakufanikiwa.

Wapo wadada warembo na wakaka wazuri tu walipendwa pia kabla yako, lakini kupendwa kwao hakukuwafanya wachagulie na huyo mume au mke wako, hivyo na wewe tambua ulipendwa lakini pia ukapata na neema ya kuchaguliwa.

Kwa hiyo unapokuwa umechaguliwa kati ya wengi waliopendwa, usifikiri kwamba wewe ni bora zaidi  kuliko hao waliochaguliwa. Mshukuru Mungu kwa hilo maana ni mapenzi yake kwako.

Tuangalie haya maneno👇

Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?) Yohana 21:20 SUV.

Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nitakapokuja, imekuhusuje wewe? Wewe unifuate mimi. Yohana 21:22 SUV.

Ukisoma katika mstari huu utaona jinsi  Yesu alivyomwambia Petro amfuate, maana yake alimchagua ili amfuate, kwa upande mwingine Petro alitaka kujua kwanini yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu hakuambiwa amfuate Yesu, isipokuwa Petro peke yake.

Inamaana hata kama Yesu alimpenda sana huyo mwanafunzi, lakini aliyemchagua amfuate ni Petro na siyo yeye, kwa hiyo unaweza kugundua kumbe kunatofauti kati ya kupendwa na kuchaguliwa.

Yesu akikuchagua tambua kwamba hiyo ni neema tu ambayo ameiachilia juu yako, wengi wanatamani kuwa kama wewe lakini hawajapata hiyo neema.

Kama umechaguliwa kati ya wengi waliopendwa kama wewe, mshukuru Mungu kwaajili ya hiyo neema na kibali alichokupatia.

Karibu kwenye darasa letu la kusoma Neno la Mungu kila siku kwa njia ya whatsApp group, tuma ujumbe wako whatsApp kwenda namba +255759808081 utaunganishwa kwenye group.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Rebecca Ernest.
www.chapeotz.com