“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”, Yn 3:16 SUV.

Andiko hili takatifu la biblia linatufunua wazi moyo na kusudi la Mungu juu ya ulimwengu huu.

Upendo wa Mungu ni mpana kiasi cha kutosha kuwakumbatia watu wote, yaani ulimwengu huu, wa kila Taifa na kabila.

“Ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli”, 1 Tim 2:4 SUV.

Upendo huu ulimfanya Mungu akamtoa mwanaye wa pekee kuwa sadaka ya dhambi msalabani. Upatanisho huu wa mwanadamu na Mungu ulikuwa ni moyo wa upendo wa Mungu ambao hakulazimishwa na mtu kufanya.

“Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?”, Rum 8:32 SUV.

Pamoja na neema hii ya Mungu bado wapo hawataki kuipokea, hawamtaki Yesu, wanaendelea kuishi maisha yasiyompendeza yeye.

Tunapaswa kuelewa wokovu ni wa kila mtu, tuliopata neema hii ya wokovu tunapaswa kuendelea kuwashawishi na wengine waungane nasi.

Mungu alitupenda kwanza, anatutaka tumwamini Yesu, na tuishi yale maisha yanayompendeza yeye siku zote za maisha yetu.

Hubiri Yesu, sema uzuri wake, tangaza matendo yake makuu waziwazi ili wenye mashaka naye waweze kumpokea kwenye mioyo yao.

Soma neno ukue kiroho
Kwetu kusoma Biblia ni maisha
Mungu akubariki sana
Samson Ernest