“Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda”, Lk 4:13 SUV.

Shetani baada ya kumjaribu Yesu na akashindwa, alienda zake kwa muda, ambapo tunamwona alirudi kwa namna nyingine kupitia Yuda na wengine.

Tunapojaribiwa na tukashinda jaribu, hatupaswi kufikiri mjaribu wetu ametuacha moja kwa moja.

Mjaribu wetu huwa haendi mbali, anakuwa karibu na kuandaa mpango mwingine wa kuja kutujaribu.

Lengo lake ni kuharibu uhusiano wetu na Mungu, anapokuja na mbinu ya kwanza akashindwa, huwa anaenda kujipanga kwa lingine.

Tunaposhinda jaribu moja hatupaswi kuishi bila tahadhari, tunapaswa kuhakikisha tunaishi vile Mungu anatutaka.

Neno la Mungu linapaswa kujaa kwa wingi mioyoni mwetu, ili mjaribu anapokuja tuweze kumtambua na kumshinda.

“Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi”, Zab 119:11 SUV.

Tujue sisi ni washindi kwenye nyakati zote zitakazotupata, ikiwa tu tutakaa kwa Bwana siku zote za maisha yetu.

Soma neno ukue kiroho
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081