Kwa maana ni nani aliyewafanya kuwa tofauti na wengine? Ni nini mlicho nacho ambacho hamkupokea? Nanyi kama mlipokea, kwa nini mnajivuna kama vile hamkupokea? 1 Wakorintho 4:7 NEN.

Moja ya misingi ya kutambua kwa mwamini, unyenyekevu wa Kikristo ni kutambua kwamba vipaji vya asili na karama za kiroho tulizonazo zinatoka kwa Mungu.

Zikiwa zinatoka kwa Mungu hazitupi nafasi ya kujivuna na kujiona sisi tunastahili kuliko wengine, na kujaa kiburi kikubwa ndani yetu.

Hadhi na umaarufu tuliopata kupitia vipaji au karama alizotupa Mungu hazipaswi kutufanya tujae viburi, kitendo ambacho ni chukizo mbele za Mungu.

Tunapaswa kuelewa vyote tulivyonavyo ni kwa sababu ya Mungu ndio maana tupo tulivyo.

Tukishaelewa hilo nafasi ya kiburi haitakuwepo kwetu, tutakuwa wanyenyekevu na kumshukuru Mungu kwa vile vipaji au vipawa na karama alivyotupa.

Changamoto inayowapata wengi hukubali kuwa na kiburi au majivuno, hii huwafanya kufarakana na Mungu wao.

Unapofarakana na mwenye Mali, uwe na uhakika ataviondoa hivyo vitu vinavyokupa kiburi.

Badala ya kuinua mabenga kwa kujawa kiburi, unapaswa kunyenyekea zaidi mbele za Mungu ili aendelee kukutumia kwenye eneo alilokujalia kuwepo.

Ukifanya hivyo maisha yako yote yatakuwa yenye kumtukuza Yesu na kumletea utukufu.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081