“Lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo”, 1 Pet 5:2 SUV.
Ukiwa mtumishi wa Mungu na kiongozi wa kanisa unapaswa kujihadhari na mambo mawili hatari;
- Kupenda Fedha, moja ya kanuni katika agano jipya kwa waangalizi au wasimamizi wa kazi ya Mungu wanapaswa kupewa kile kiwango kinachokidhi mahitaji yao na familia zao.
Kile kiasi wanachopewa wanapaswa kuridhika nacho na kuepuka kujiingiza kwenye tamaa mbaya ya fedha ambazo zitapelekea kumkosea Mungu wao.
Wale watumishi wanaoanguka katika jambo hili la fedha, wanajiingiza kwenye matatizo mabaya na wanajipatia dhambi mbele za Mungu.
Wale ambao huanza kuchukua pesa ya kanisa bila utaratibu kufanyia mambo yao, na kuchukua fedha za washirika wao bila utaratibu, na hawarudishi, hujipatia hatia mbele za Mungu.
- Kupenda ubwana, wapo watumishi wanapenda madaraka, uchu wao wa madaraka hupelekea kutumia nguvu nyingi na kuongoza vibaya.
Mchungaji anapaswa kuwa kielelezo chema kwa kundi na kujitoa kwa Kristo katika utumishi wenye unyenyekevu, uvumilivu katika haki, ujasiri, uthabiti katika maombi, kukemea dhambi, kulipenda neno la Mungu, na kuwaelekeza waamini katika njia sahihi.
Ukitenda hivi na kuishi maisha yanayompendeza Mungu, utumishi wako hautalaumiwa na utakuwa mwema mbele za Mungu, na utaacha alama njema.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana
Samson Ernest