“Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida”, 1 The 3:5 SUV.
Ukisoma 1 The 2: 18 katika sura tuliyosoma jana utaona mtume Paulo amerudia mara ya pili kutaja shughuli za Shetani.
Inaonyesha wazi kuwa Paulo alitambua na kuamini uwepo wa Shetani na milki ya pepo wabaya.
“Ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi”, Efe 2:2 SUV.
Siku hizi sio ajabu kuona wapo watu hawaamini kabisa kama kuna uwepo wa Shetani.
Utaona ni mara chache Shetani anatajwa, na kama atatajwa, utaona anatajwa kama vile ni kitu kisicho na madhara au kisichoweza kuleta madhara kwa mwamini.
Wengine wamemweka Shetani kwenye kundi ambalo anaonyesha sio adui yetu, waona haina haja kukemea mapepo yanayowatesa watu.
Yesu alitoa pepo wabaya kwa watu waliokuwa wanasubuliwa nayo, ikiwa kuna watu wataona Shetani hana madhara yeyote na kumwacha aendelee kuwatesa watu tutakuwa tunakosea.
Ukiona kuna kanisa halimpingi Shetani, unapaswa kufikiri vizuri, maana huyu ni adui yetu mkubwa anayetuwinda usiku na mchana.
“Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake”, Mt 4:10 SUV.
Shetani lazima asemwe na watu wajue yupo, wajue wasipokuwa makini wakaenda pasipo kujilinda watajikuta wameingia kwenye maisha yasiyompendeza Mungu.
Mbinu zake ni nyingi, ukiwa unavutwa kufanya mambo mengine ila ukitaka kuomba unashindwa, ukitaka kusoma neno unashindwa, ukitaka kwenda ibadani unasikia mzito ujue umevamiwa.
Hakikisha unajiimarisha kupitia mafundisho, maombi na kusoma biblia na kutafakari, hii itakusaidia kujengeka vyema kiroho.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081