Unajua kuna vitu vingine vinasikitisha sana ndugu zangu, sijui ni utoto au ulimbukeni unatusumbua vijana wa leo.

Kaka/dada anakutana na mdada/mkaka wakapendana huko na wakakubaliana ya kukubaliana, bila kukaa chini akatulia kujua maamzi aliyofanya juu ya mwenzake ni sahihi au amekurupuka.

Bila kukaa chini kupanga hatua za msingi za kufuata ili wazazi/walezi wote wa pande mbili watambue uhusiano wao.

Wao wanaanza mbwembwe, mbwembwe ambazo ukiziangalia unaona kabisa huu ni usanii usanii ambao mwisho wake ni maumivu makali sana kwa mmoja wao.

Sio kila anayekuja kwako kuanzisha mahusiano ana nia ya kweli kukuoa, sio kila unayemwona kwako anafaa kuoa ana nia ya kweli umwoe. Wengine wanakuja kwako kupoza maumivu waliyoumizwa na wapenzi wao wa nyuma, baada ya hapo wanaweza kurudiana nao.

Wengine wanakuja kwako ili wapoze tamaa zao za mwili, wengine wanakuja kwako kwa sababu wanajua uchumi wako upo vizuri. Kama uchumi upo vizuri wanataka uwe kitega uchumi chao, lakini hawana mpango wa kuishi na wewe.

Sasa wewe dada, kaka akija kwako akakutamkia anakupenda na anataka kuishi na wewe unaaza kumwanika kila kona, hujachukua hata mwezi mmoja umjue kama kweli anamaanisha alichokisema, wala hujachukua muda kujua uhusiano wake na Mungu ukoje, wewe kwa sababu una kiu ya kuolewa/kuoa basi unaona kila kitu kipo sawa.

Tuache utoto kwenye mambo ya msingi, jihakikishie uliyenaye kwanza ni mtu sahihi wa kuwa naye au ana ageda yake binafsi. Wengine sio waoaji, wengine sio waoelewaji, wengine wapo wapo tu.

Hebu tulia, acha kuendesha mambo kwa mihemko ya kuwaonyesha wale waliokuumiza na wewe sasa unaye, nakwambia atakuumiza na huyo ndipo utaanza kujidharau. Maana utaanza kuchekwa kwa jinsi ulivyokuwa unawaonyesha wenzako mbwembwe.

Mtu hajakutolea hata mahari, mtu hujamtolea mahari, kila kona unataka watu wamjue, wakati mwingine anakuhurumia jinsi unavyojiharibia jina maana yeye mwenyewe hana mpango wa kuoa/kuolewa na wewe.

Acha mbwembwe, nenda kwa akili na mipango inayomshirikisha Mungu mpaka uhakikishe umejua mtu uliyenaye kweli anamaanisha kile ulichokitamka/alichokitamka kwako.

Mungu akubariki sana kwa muda wako.

Chapeo Ya Wokovu.

+255759808081.