Kinachofanyika kwa mtu, labda uponyaji juu yake na madaktari walishindwa kumsaidia apone huyo mtu. Na mtu huyo Mungu akamponya ugonjwa uliokuwa unamsumbua kwenye mwili wake.

Kitendo hicho ni kudhihirisha ukuu wa Mungu kwa mwanadamu, kile kimeshindikana kabisa alafu Mungu akajitokeza katikati. Ujue Mungu anapaswa kuinuliwa katika hilo.

Kama mwanadamu angeweza jambo hilo, na anajua hata bila Mungu anaweza akatoa msaada au akafanya. Anaweza asijue sana uweza wa Mungu juu ya maisha yake.

Yapo mambo yanafanyika kwetu wanadamu ili wengine waweze kujifunza jambo jema la kumkimbilia Yesu Kristo tu.

Rejea: Watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa BWANA, ya kuwa ni mkono wenye uweza, ili wamche BWANA, Mungu wenu, milele. YOS. 4:24 SUV.

Hilo ni kusudi la Mungu haswa katika maisha ya mwanadamu, Mungu wetu anajitambulisha kwetu kwa namna tofauti tofauti zenye nguvu.

Yapo mazingira watu wanaweza wasijue uweza wa Mungu hadi waone jambo fulani limetendeka mbele ya macho yao. Au kwenye maisha yao binafsi.

Unaweza usijue sana umhimu wa kumcha Bwana katika maisha yako kama hujaona kitu fulani maalum sana kwenye maisha yako.

Pale Mungu anapokuonekania, au unapoona amemuonekania mtu unayemfahamu, unapata kiu zaidi ya kumjua Mungu wa kweli zaidi na zaidi.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
www.chapeotz.com