“Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga”, Yn 13:5 SUV.

Kitendo hiki cha kuvutia cha Yesu kuwatawadha wanafunzi wake miguu kilitokea usiku wa mwisho wa maisha yake hapa duniani.

Yesu alifanya jambo hili kwa madhumuni yafuatayo;

Moja, kuwaonyesha wanafunzi wake ni kwa jinsi gani aliwapenda wao.

Pili, aliashiria kujidhabihu kwake msalabani muda mchache ujao.

Tatu, kuwasilisha ukweli kwamba alikuwa anawataka wanafunzi wake kutumikiana wao kwa wao kwa unyenyekevu mkubwa.

Yesu aliwataka waone kwamba tamaa ya kuwa wa kwanza, na kuheshimiwa zaidi ya wakristo wengine ni kinyume cha roho ya Bwana wao.

‘Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema”, 1 Pet 5:5 SUV.

Tunapaswa kutumikiana na kuheshimiana kwa kila mmoja wetu kwa unyenyekevu mkubwa, tukishindwa kufanya hivyo tutakuwa mabwana wa kutaka kutukuzwa.

Yesu anatufundisha somo kubwa sana kwa waamini wote wa leo, tunapaswa kuheshimiana na kumwona kila mmoja ni wa thamani mbele za Bwana.

Soma neno ukue kiroho
Kwetu kusoma biblia ni maisha
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081