Kila mmoja Mungu ameruhusu azaliwe na mzazi wake kwa kusudi maalum.

Haijalishi umezaliwa na mzazi yukoje ila fahamu kwamba ndiye Mungu ameruhusu uzaliwe na mzazi huyo.

Haijalishi unajua ama hujui kuwa Mungu amekuleta duniani kwa kusudi maalum.

Lakini napenda ufahamu kwamba, una jambo la kufanya hapa duniani.

Jambo lenyewe sio kana kwamba lipo mbali sana na wewe, ni maisha yako ya kila siku unayoishi.

Katika kazi yako unapaswa kuifanya kwa kiwango kikubwa sana, kiasi kwamba hapaswi kutokea mtu mwingine kama wewe.

Katika huduma yako ambayo Mungu amekupa katika maisha yako. Unapaswa kuifanya kwa nguvu zako zote, kwa akili zako zote, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote.

Ule umaalum/upekee wako Mungu aliokupa au alioweka ndani yako. Unapaswa kuutumia sawa sawa.

Kufanya hivyo utaleta utofauti wako na watu wengine watakaokuja nyuma yako, na watakaofuata mbele yako.

Hili tunaliona kwa Musa mwenyewe, hakuinuka nabii mwingine katika Israel kama Musa.

Rejea: Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye BWANA alimjua uso kwa uso; KUM. 34:10 SUV.

Hata wewe unaweza ukamtumikia Mungu kwa viwango ambavyo ameviweka ndani yako.

Kupitia viwango ambavyo utamtumikia, na kupitia upekee ambao Mungu amekuumbia ndani yako. Unaweza kuandika historia yako yenye upekee.

Mungu akusaidie uweze kulitimiza kusudi la Mungu la  kukuleta hapa duniani, ili watu wakose mtu wa kukulanganisha naye.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
www.chapeotz.com