Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula. Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe. Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu, basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu”, Mt 15:2‭-‬6 SUV.

Katika maandiko haya inaonyesha wazi kuwa baadhi ya Mafarisayo walipuuza amri za Mungu kwa sababu ya mapokeo yao waliyoyapokea kutoka kwa wazee wao na yalikuwa mawazo ya kibinadamu yaliyo kinyume na Mungu.

Hii inatuweka wazi hata siku za leo, waamini wanapaswa kuwa makini sana na wawe na macho ya rohoni wasije wakalitangua Neno la Mungu kwa sababu ya mapokeo ya jamii zao au wazee wao.

Hasa yale mawazo yanayopendwa na watu wengi kutokana na kawaida za utamaduni wao wa kisasa, ama uliozoeleka kutoka kwa mababu na mababu ila upo kinyume na neno la Mungu.

Tukisema hatuwezi kuyaacha mapokeo ya wazee wetu bali tutayaenzi, tukafanya kama mapokeo yanavyotutaka, tufahamu kuwa kufanya hayo ni kuanguka katika dhambi hii ya Mafarisayo na viongozi wa Kiyahudi.

Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu”, Mk 7:8 SUV.

Yapo mapokeo hatupaswi kuyaenzi tukishaokoka, haijalishi jamii au familia au koo zetu zitatuchukuliaje, mambo yote yanayomkosea Mungu au yaliyo kinyume na neno lake hatupaswi kuyatenda.

Tukiona mapokeo yetu ni ya muhimu zaidi kuliko neno la Mungu tujue tutakuwa tunamtenda Mungu dhambi huku tukisema tumeokoka, na tutakuwa mbali na uwepo wa Mungu.

Lazima tujitofautishe baadhi ya maeneo, yapo mapokeo tunapaswa kuyakataa kabisa, hasa yale yanayopelekea kumtenda Mungu dhambi, haijalishi wengi wanapenda, maana tunajua athari zake ni kubwa.

Zipo tamaduni zetu, ndani yake kuna mambo mengi sana kutokana na makabila yetu, humo ndani kunakuwa na mambo ambayo ni uchafu na dhambi mbele za Mungu, tukishaijua kweli hatupaswi kuendelea nayo.

Yale mapokeo mazuri tuende nayo, yale yaliyo kinyume na neno la Mungu tukae nayo mbali, haijalishi yanapendwa na kuthaminiwa na wengi, sisi tuyakatae na kuliishi neno linavyotutaka tuishi.

Mwisho, nikualike kwenye kundi la wasap lililo na watu wengi wanaosoma neno la Mungu kila siku na kutafakari na kupata mafundisho mbalimbali, wasiliana nasi kwa wasap +255759808081, utaunganishwa kwenye kundi hili zuri.

Soma neno ukue kiroho

Mungu akubariki sana

Samson Ernest