Umuhimu Wa Kujua Mila Na Desturi Za Unayetaka Kumuoa/Kuolewa Naye.
Tunapompokea Yesu anatubadilisha mambo mengi sana, namna isiyofaa mbele zake inaondoka ndani mwa mtu hasa pale anapojazwa na Roho Mtakatifu. Unakuta mnakuwa kitu kimoja na watu ambao hamkuzaliwa tumbo moja na wala sio wa kabila moja. Pamoja na hayo yapo mambo katika tamaduni zetu huwa hayaachwi moja kwa moja, ndio maana utaambiwa mambo fulani yameondolewa [...]