Sio jambo la kushangaa mtu kupata kile alikuwa anapambana usiku na mchana kukipata.

Baada ya kukipata hicho alichokuwa anakitafuta sana kwenye maisha yake.

Badala ya kuleta amani/furaha ya moyo wake au kwenye maisha yake.

Kujibiwa kwake hitaji lake kukamletea huzuni ndani ya moyo wake.

Yupo anaweza akawa amepitia njia zisizo sahihi, kwahiyo atakapopata lile alikuwa analihitaji.

Mtu huyo anaweza asiwe na raha yeyote kwenye maisha yake.

Uzuri wa Mungu kujibu maombi yako, uzuri wa Mungu kukupa lile ulikuwa unahitaji.

Raha yake itaambatana nawe, utajisikia vizuri moyoni mwako kutokana na lile Mungu ametenda kwako.

Hili tunajifunza kwa wana wa Israel baada ya kugawiwa maeneo yao.

Kila mmoja alipokea raha ya Bwana kwenye maisha yake, yale maeneo aliyopewa yalikuwa baraka kwake.

Rejea: Kisha BWANA akawapa raha pande zote, sawasawa na hayo yote aliyokuwa amewaapia baba zao; wala katika adui zao wote hakusimama hata mtu mmoja miongoni mwao mbele zao; yeye BWANA akawatia adui zao wote mikononi mwao. YOS. 21:44 SUV.

Itakuwa ajabu kama Bwana amekupa jambo fulani, inaweza ikawa kazi, mtoto, na mengine mengi.

Alafu ukakosa amani ya moyo wako, hali hiyo itakusababisha usione umhimu wa Mungu kukupa kile ulimwomba.

Tunapaswa kuwa na amani/raha baada ya Mungu kutupa yale mahitaji yetu.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest
www.chapeotz.com