FIKIRI ZA SIKU – Page 2 – Chapeo Ya Wokovu

FIKIRI 21; SIKU AKIKUTANA NA MWINGINE.

Kazi yako unayoifanya kwa wengine, labda wewe ni fundi nyumba, au fundi cherehani, au fundi umeme, au fundi telisi, na ufundi mwingine mwingi ambao sijautaja hapa. Unafikiri huduma unayotoa kwa wateja wako ni ya uhakika? Unafikiri huyo mteja wako akikutana na fundi mwingine akafanyiwa kazi uliyomfanyia wewe, atakukumbuka na kukuona wewe bado fundi bora kwake? [...]

By | February 18th, 2020|FIKIRI ZA SIKU|0 Comments

FIKIRI 20; UMEHUSIKA VIPI.

Tunaweza tukawa watu wazuri sana wa kuwalalamikia wengine kwa kufanya mambo yasiyofaa, mambo ambayo ni chukizo kwa Mungu wetu. Ninachoweza kukuambia leo, katika hilo unaloona halipo sawa wewe kama wewe umehusika vipi kuhakikisha kitu kama hicho hakitokei. Elimu gani umeitoa kuhakikisha hicho kilichotokea hakitokei kwa mtu aliyepita kwenye mikono yako au kwenye ushauri wako? Kipi [...]

By | February 16th, 2020|FIKIRI ZA SIKU|0 Comments

FIKIRI 19; UNAPATA FAIDA GANI.

Sifikiri kama kuna mtu anaweza kufanya kitu bila kutegemea kupata faida, hata mtu anayeua wengine atakuwa anategemea kupata kitu fulani baada ya kufanya hivyo. Ikiwa mtu anafanya kitu au jambo kwa kutegemea faida, au kutegemea kupata matokeo fulani mazuri kwa manufaa yake, au kwa manufaa ya wazazi wake, au kwa manufaa ya watoto wake, au [...]

By | February 15th, 2020|FIKIRI ZA SIKU|0 Comments

FIKIRI 18; IMEKUSUDIWA UKOSE/USIPATE.

Kila mmoja wetu kuna vitu anatamani viwe sehemu ya maisha yake au anatamani avifikie au avipate. Katika kutaka kuvipata anakuwa anapambana kufikia kile anakitaka. Katika kupambana huko anashangaa lile alilolikusudia kulipata linaenda kwa mtu mwingine au halioni kabisa limepotelea wapi. Mungu wetu ni mwema Sana, unaweza ukalaumu sana kwanini hukupata kile ambacho ulikitaka/ulikitarajia kiwe sehemu [...]

By | February 14th, 2020|FIKIRI ZA SIKU|0 Comments

FIKIRI 17; JE AMEKOSEA KUKUPA?

Kuna vitu huwa tunavifanya utafikiri kuna shida imetokea kwenye fahamu zetu, kumbe ni wazima kabisa wa afya njema. Mtu anakujia kwako akiwa na shida kabisa, wakati mwingine anatoa na machozi kabisa. Unamhurumia na kumsaidia kile kiasi alikuwa anahitaji kutoka kwako umwazime kwa kukuahidi atakurudishia siku/mwezi fulani. Unafika ule wakati ambao alikuahidi kwa kinywa chake, ukipiga [...]

By | February 13th, 2020|FIKIRI ZA SIKU|0 Comments

FIKIRI 16; KINACHOMFANYA UMCHUKIE.

Katika maisha yetu haya, bila shaka umewahi kukumbwa na hali ya kumchukia mtu fulani aliyekuumiza au aliyekutenda jambo baya. Wapo wengine tumewahi kujikuta au tumejikuta tunawachukia kwa kuambiwa na watu wengine. Bila kuwa na uhakika na taarifa tulizopewa, tunajenga chuki juu yao. Leo napenda ujifunze jambo hapa, ujumbe huu utakufikirisha kwa kina zaidi ili usiwe [...]

By | February 12th, 2020|FIKIRI ZA SIKU|0 Comments

FIKIRI 15; SIKU YAKO…

Ili siku yako iishe kwa ushindi, uone moyoni mwako kuwa siku ya leo imepita vizuri na kuna kitu umefanya cha maana sana. Vitu gani huwa ukifanya unajisikia vizuri moyoni mwako, hata kama kwa kujilazimisha kufanya jambo ambalo mwili wako hutaki kabisa siku hiyo. Lazima kuna vitu ambavyo tukivifanya huwa tunajisikia vizuri, tunaona siku yetu tumeimaliza [...]

By | February 7th, 2020|FIKIRI ZA SIKU|0 Comments

FIKIRI 14; KWANINI WAMEKUAMBIA HIVYO.

Kuna kitu kinaweza kikatokea ukaambiwa maneno fulani ya kukuumiza moyo wako. Wanaweza wakawa wanasema kweli au wanaweza wakawa wanaongea maneno ya uongo. Anaweza akatokea mtu akakuambia maneno ambayo kwako yakawa na maswali mengi au yakazua sintofahamu kwako. Ninachotaka ukielewe hapa na ufikiri zaidi ni kwamba kwanini wakuambia hayo waliyokuambia. Uwe umefurahi, ama uwe hujafurahi, kipi [...]

By | February 6th, 2020|FIKIRI ZA SIKU|0 Comments

FIKIRI 13; AMEPATAJE NGUVU/UJASIRI KWAKO.

Kitu ambacho tunaweza tusikijue sana katika maisha yetu ni kwamba wapo watu wanapata ujasiri wa kuongea yale mambo magumu kwetu, kwa sababu ipo nguvu ambayo ipo nyuma yao inayowafanya hivyo. Unaweza ukaumiza kichwa sana na kujiuliza huyu mtoto amepata wapi ujasiri wa kuja kuniambia haya maneno. Kumbe yupo aliye na nguvu nyuma yake, anayemfanya apate [...]

By | February 5th, 2020|FIKIRI ZA SIKU|0 Comments

FIKIRI 12; ULIVYOKUWA NYUMA NA SASA.

Ulivyokuwa nyuma inaweza isifanane kabisa na sasa ulivyo, inawezakana kabisa ulivyokuwa nyuma ni afadhali kuliko sasa. Inawezekana ulivyo sasa ni hatua kubwa sana kuliko ulivyokuwa huko nyuma, na inawezakana ulipo sasa umeshuka sana kuliko huko nyuma. Inawezekana kiwango chako cha ukuaji kiroho kimeongezeka sana kuliko huko nyuma, na inawezekana kiwango chako cha kiroho kimeshuka sana [...]

By | February 3rd, 2020|FIKIRI ZA SIKU|0 Comments

Watch Dragon ball super