Je, Mungu Akiamua Kutoa Ushahidi Wake Kwako Utabaki Salama Au Utahukumiwa?
"Nena na wana wa israeli, uwaambie, kama mke wa mtu ye yote akikengeuka, na kumkosa mumewe, na mtu mume akalala naye kwa uasherati, na jambo hilo likamfichamania mumewe, likawa jambo lisilojulikana, na huyo mwanamke akawa najisi, wala hapana shahidi aliyeshuhudia juu yake, wala hakufumaniwa", Hes 5:12-13 SUV. Uliwekwa utaratibu kwa Waisraeli, yule mwanaume ambaye alimdhania [...]