Neno La Leo – Chapeo Ya Wokovu

Kiwango Chako Cha Kumpenda Mungu Kinaamua Maisha Yako Yaweje.

Wakati mwingine tumekuwa tunamwendea Mungu tukiwa na shida, tunakuwa siriazi kweli kumweleza shida zetu. Kufanya hivyo sio vibaya kwa upande mwingine ila kwa upande mwingine kuna shida, yaani ni sawa kumkumbuka mtu wakati wa shida ila wakati huna shida upo na mambo yako. Kumpenda Mungu kwa misimu, yaani ukiwa muhitaji wa jambo fulani kwake ndio [...]

By | July 13th, 2020|Neno La Leo|0 Comments

Anza Na Bwana Kwa Kile Ulicho Nacho.

2 FAL. 4:2 SUV. Elisha akamwambia, nikufanyie nini? Niambie una kitu gani nyumbani? Akasema, mimi mjakazi wako sina kitu, ila chupa ya mafuta. Kila mmoja ana kitu cha kuanzia ili aende hatua nyingine. Hicho hicho uonacho si kitu, ndicho Bwana anataka kuanza nacho. Huyu mke wa mtumishi alikuwa anapita kwenye changamoto nyingi; ujane, umaskini, upweke [...]

By | July 11th, 2020|Neno La Leo|0 Comments

Mawazo Ya Mungu Si Kama Ya Mwanadamu.

Maandiko yanatuambia kwamba; Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. ISA. 1:18 SUV. Wekundu wa dhambi yako unaweza ukawafanya watu wakuhukumu na kuona kwamba dhambi yako haiwezi kusamehewa. Lakini sivyo Mungu anavyomtazama mtu huyo, Mungu anapokuwa kwenye kiti cha enzi anatamani [...]

By | July 7th, 2020|Neno La Leo|0 Comments

Madhara Ya Kumwangamiza/Kumwondoa Mtu Kwa Hila Ili Wewe Umiliki Nafasi/Eneo Lake Halali.

Katika maisha haya, Mungu anaweza kumfanikisha mtu mali nyingi, anaweza akawa na mashamba ya kutosha, anaweza akawa na nyumba za kutosha, anaweza akawa na fedha nyingi, na vingine vingi vinavyofanana na hivyo. Mtu mwingine anaweza akawa na nafasi kubwa kwenye jamii yake inayomzunguka, anaweza akawa ni kiongozi kwenye nafasi fulani nyeti serikalini. Ambayo hiyo nafasi [...]

By | July 4th, 2020|Neno La Leo|0 Comments

Majaribu Hayaangalii Mungu Amekutumia Kwa Kiwango Gani.

Tunapojifunza Biblia tunaona jinsi Yesu mwenyewe wakati ametoka kwenye maombi ya siku arobaini, tunaona jinsi Shetani alikuja na kumjaribu. Pamoja na yale maombi ya siku arobaini hayakuweza kuzuia majaribu yasimkute Yesu, lakini ni kwa sababu kazi ya majaribu ni kumuimarisha mtu, ndio maana huwezi kuyazuia yasije kwako. Kuna shuhuda nyingi tu watumishi wa Mungu wanashuhudia [...]

By | July 2nd, 2020|Neno La Leo|0 Comments

Mungu Anaweza Kukurejeshea Tena Kile Ambacho Ulikipoteza.

Kuna vitu katika maisha yetu tunaweza kuvipoteza kwa kushindwa kutii maagizo tunayopewa na Mungu. Tunapovipoteza wengi huwa tunabaki tunaumia, wengine hubaki kulalamika, wengine hubaki kulia, wengine hufikiri kujiua. Wapo wengine huacha wokovu, hasa pale wanapoona sifa yao imekuwa mbaya. Badala ya kutubu na kunyenyekea mbele za Mungu, huwa wanaona njia rahisi ni kuacha wokovu. Wengine [...]

By | June 29th, 2020|Neno La Leo|0 Comments

Kuacha Ushauri Mzuri Na Kufuata Ushauri Mwingine Usiofaa.

Wengi sio wageni na neno hili ushauri, ni neno ambalo tunalisikia kila mara, haitoshi tu kulisikia, inawezekana kabisa tumewahi kutoa Ushauri, au kupewa ushauri na wengine. Inawezekana ni wazazi wako, au ndugu zako, au jamaa zako, au rafiki zako, au viongozi wako, walikupa ushauri ambao ulikuwa unauhitaji. Kuna ushauri wa kuomba wewe, unaenda kwa mtu [...]

By | June 28th, 2020|Neno La Leo|0 Comments

Maombi Yako Yanaweza Kujibiwa Na Mungu Lakini Kuna Ziada Unayopata Ukienenda Sawa Sawa Na Mapenzi Ya Mungu.

Kwanza unapaswa kufahamu Mungu wetu ni mwaminifu sana, kwanini nasema ni mwaminifu? Lile ambalo umemwomba atakupa. Ukiomba na ukiamini uwe na uhakika Mungu anaweza kukujibu maombi yako, bila kujalisha hilo jambo lina ukubwa gani. Katika kujibiwa huwa kunaleta faraja, huwa kunaleta furaha, huwa mtu anakuwa na ushuhuda mkubwa sana wa kuwashirikisha wengine. Pamoja na kujibiwa [...]

By | June 25th, 2020|Neno La Leo|0 Comments

Fahamu Lugha Ya Fumbo Anapozungumza Kiongozi/Mzazi Wako.

Mtu anapokuwa mkubwa, anaweza akawa mzazi wako, au anaweza akawa kiongozi wako kazini kwako. Akakueleza kuwa ana uhitaji wa kitu fulani bila kukuambia wewe ndiye unapaswa kumletea, ukiwa kama mtenda kazi wake, ama ukiwa kama mtoto wake. Unapaswa kuchukua hatua ya haraka kumletea kile ambacho ana uhitaji nacho. Mara nyingi mtu anapokuwa na nafasi fulani, [...]

By | June 17th, 2020|Neno La Leo|0 Comments

Kinachotufanya Tufanye Mambo Makubwa.

Yapo mambo mengi sana huwa tunafanya hadi mtu anafika wakati anajishangaa mwenyewe vile anafanya mambo. Kama sio yeye kujishangaa, wale wanaomzunguka wanakuwa wanamshangaa vile anafanya mambo makubwa. Wakati mwingine watu wanakuwa na shauku ya kutaka kufahamu nini chanzo cha kuweza kufanya hayo. Wapo wanaotambua uwezo mkubwa, au mambo makubwa wanayoyafanya hadi ulimwengu unashangaa. Yupo anayewawezesha [...]

By | June 15th, 2020|Neno La Leo|0 Comments

Watch Dragon ball super