Neno La Leo – Page 2 – Chapeo Ya Wokovu

Chimba Ukate Mizizi Na Shina La Uchungu Ndani Yako

"Mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo", Ebr 12:15 SUV. Shina la uchungu humaanisha roho na hali ya uhasama na chuki kali iliyo ndani ya mtu. Hali hii inaweza ikawa kumwelekea Mungu au iliyosababishwa na matendo mabaya aliyotendewa mtu. Uchungu husababishwa [...]

By | March 4th, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Mwenye Haki Wa Mungu Ataishi Kwa Imani

"Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye", Ebr 10:38 SUV. Moja ya kanuni muhimu kwa mwamini na iliyothibitishwa na maandiko matakatifu ni hii ya Imani, ukisoma Habakuki 2:4, Warumi 1:17, Wagalatia 3:11, Waebrania 10:38 utaona Imani inazungumzwa sana kwa mwamini. Pasipo Imani hatuwezi kumpendeza Mungu, Imani hutufanya tuwe [...]

By | March 2nd, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Mungu Habadiliki Na Hawezi Kusema Uongo

"Ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu", Ebr 6:18 SUV. Moja ya sifa kuu aliyonayo Mungu wetu ni habadiliki na hana ahadi za uongo, lile aliloliahidi kwetu kupitia neno lake atalitimiza sawasawa na mapenzi yake. Mtu anaweza [...]

By | February 25th, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Hawataingia Katika Raha Yake Ya Milele

"Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arobaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, ila wale walioasi? Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao", Ebr 3:17‭-‬19 SUV. Wale waamini wanaoenda kinyume na Mungu kuna uwezekano wa kuikosa [...]

By | February 22nd, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Siwezi Kumnyenyekea Mtu Namnyenyekea Mungu Peke Yake

"Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote" Tit 3:1‭-‬2 SUV. Moja ya kauli zetu tunazotoa kuonyesha wazi kutowaheshimu watu wenye uwezo na mamlaka waliyonayo kwenye jamii au kanisa ni hii. Tumejikuta [...]

By | February 17th, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Uwe Mvumilivu Katika Kuitenda Kazi Ya Mungu

"Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu", 2 Tim 2:3 SUV. Watu wanaoitenda kazi ya Bwana yaani kuihubiri injili na kutumika hemani mwa Bwana wanatakiwa kuwa wavumilivu katika magumu yote wanayokutana nayo. "Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi", 2 Tim 2:9 SUV. Tukiwa Askari [...]

By | February 11th, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Mtu Mwenye Imani Thabiti Isiyokuwa Na Unafiki

2 Timotheo 14 Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha; 5 nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo. Paulo akiwa amefungwa gerezeni huko Rumi akisubiri kifo, wakati huo marafiki zake wengi wakiwa wamemwacha alimwandikia Timotheo [...]

By | February 10th, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Usimwekee Mtu Mikono Kwa Haraka Kwenye Utumishi

"Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi", 1 Tim 5:22 SUV. Kusimikwa kwa wazee wa kanisa au watumishi wengine Paulo anasisitiza mambo kadhaa; 1. Mtu yeyote asisimikwe katika nafasi ya uzee au uinjilisti au ushemasi au uchungaji kwa haraka. Sharti hili na mwongozo huu wa Maandiko [...]

By | February 8th, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Sifa Ya Mtu Anayetaka Kuwa Askofu Au Mwangalizi

"Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha", 1 Tim 3:2 SUV. Zipo sifa mbalimbali kwa kila eneo la kazi au huduma husika, sifa hizo zinamfanya mtu ajichunguze mwenyewe kama anakidhi vigezo ama la. Nje na elimu ya mtu juu ya kazi husika, [...]

By | February 6th, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Shetani Kupewa Watu Awafundishe Tabia Njema

"Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu", 1 Tim 1:20 SUV. Linaweza likawa neno la kushangaza kusikia Shetani amepewa watu awafundishe, Shetani ambaye tunamjua ni baba wa uovu Leo hii anakabidhiwa watu awafundishe. Paulo kuwakabidhi waamini kwa Shetani inaonyesha walishindikana kabisa kutokana na tabia zao mbaya mbele [...]

By | February 3rd, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Watch Dragon ball super