Neno La Leo – Page 3 – Chapeo Ya Wokovu

Usiambatane Na Watu Wasiopenda Kufanya Kazi

"Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu", 2 The 3:6 SUV. Watu wasio na utaratibu waliosemwa hapa ni wale watu waliokuwa wanazurura na hawakupenda kufanya kazi. Walichokuwa wanafanya ni kuwa walitumia vibaya ukarimu wa kanisa na walipokea misaada [...]

By | February 2nd, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Uwe Macho Usije Ukaingia Kwenye Mikono Ya Mjaribu

"Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida", 1 The 3:5 SUV. Ukisoma 1 The 2: 18 katika sura tuliyosoma jana utaona mtume Paulo amerudia mara ya pili kutaja shughuli za Shetani. Inaonyesha wazi kuwa Paulo alitambua na kuamini [...]

By | January 27th, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Changamoto/shida Unayopitia Isikuzuie Kulitumikia Kusudi La Mungu

"Salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni kufungwa kwangu. Neema na iwe pamoja nanyi", Kol 4:18 SUV. Tumezoea kuona mtu akiwa anapitia shida au changamoto fulani huacha kufanya mambo ya muhimu aliyokuwa anayafanya hapo awali. Mtu anaona bora kupumzika au kuacha kabisa hadi pale atakapokaa sawa, jambo ambalo linaweza kumrudisha nyuma zaidi. Zipo [...]

By | January 24th, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Jukumu Lolote Utakalopewa Au Litakalopita Kwenye Mikono Yako Lifanye Kwa Moyo Wako Wote

"Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo", Kol 3:23‭-‬24 SUV. Mtume Paulo anawasihi sana Wakristo wahesabu kazi zote kuwa ni huduma inayotolewa kwa Bwana Yesu. Tunapaswa kufanya kazi kana kwamba Yesu Kristo ndiye Mwajiri wetu, tukijua kazi [...]

By | January 23rd, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Tupo Huru Katika Kristo Ila Sio Huru Wa Kufanya Kila Jambo

"Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo", Gal 5:13 SUV. Mtume Paulo aliwakumbusha Wagalatia jambo la muhimu sana kuhusu uhuru walioupata kwa kumwamini Yesu Kristo. Uhuru huu haukuwa wa kufanya kila kitu, uhuru uliozungumzwa hapa ulikuwa wa kutoka katika utumwa wa dhambi na wa [...]

By | January 6th, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Tofauti Zetu Zimeondolewa Na Mungu Wote Ni Sawa Mbele Zake

"Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu", Gal 3:28 SUV. Hapa Paulo aeleza wazi na kuondoa tofauti zote za kikabila, kirangi, kitaifa, kijamii na kijinsia kuhusu uhusiano binafsi wa mtu na Yesu Kristo. Ile Mimi wa kabila fulani, Mimi wa [...]

By | January 4th, 2023|Neno La Leo|0 Comments

Usikubali Shetani Akushinde Kwa Namna Yeyote Ile

"Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake", 2 Kor 2:11 SUV. Moja ya silaha muhimu kwa mwamini ya kumshinda Shetani ni kuzitambua hila zake. Huwa tunaingia kwenye mitengo mibaya ya Shetani kwa kushindwa kuzitambua hila zake mbaya. Jambo linaweza kuanza kama utani, usipokuwa na jicho la rohoni ukaliepuka hilo jambo, litakuingiza kwenye [...]

By | December 19th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Kupita Katika Kipindi Cha Kukata Tamaa Ya Kuishi

"Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi. Naam, sisi wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye wafu, aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena atatuokoa; ambaye tumemtumaini kwamba [...]

By | December 17th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Wanawake Na Wanyamaze Katika Kanisa

Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo. 1 Kor 14:34 SUV Mstari huu unatafasiriwa vizuri na mstari unaofuata wa 35, kwanini wanawake wanaambiwa wanyamaze. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa. 1 Kor [...]

By | December 14th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Sote Tumebatizwa Kwa Roho Mmoja

"Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja", 1 Kor 12:13 SUV. Ubatizo huu wa roho mmoja hauna maana kuwa ni ubatizo wa maji au Kristo kuwabatiza waamini katika Roho Mtakatifu kama ilivyokuwa [...]

By | December 12th, 2022|Neno La Leo|0 Comments

Watch Dragon ball super