Ushuhuda Wa Jinsi Mungu Amenitendea Kupitia Chapeo Ya Wokovu
Mch Samson; Shalom mtu wa Mungu! Wewe unajua kuanza kwangu Chapeo ya Wokovu hata hapa Mungu aliponifikisha, na mbele ninaendelea kwa msaada wa Mungu. Bado najiona sitoshei katika kujifunza Neno la Mungu, lakini Mungu ananishangaza sana na siwezi kuendelea kunyamaza. Mwaka jana July, nilipewa jukumu na Mchungaji wangu kuwa nafanya maandalio ya masomo kupitia kile [...]