
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo aliye hai, Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa uzima wake ambao anaendelea kunipa, na hii nafasi ya kuendelea kutukutanisha na wewe.
Kunyamaza ni nzuri sana, na vile vile kunyamaza ni mbaya sana, upo wakati unapaswa kunyamaza kimya. Na upo wakati unapaswa kutonyamaza kimya.
Kwanini nasema hivi, hebu fikiri ungenyamaza kimya ungeepusha mambo mangapi kwenye jambo ambalo limetokea kwako.
Na sasa ukiangalia madhara yaliyotokea ni makubwa baada ya kunyanyua kinywa chako kuanza kujibizana kwa maneno na aliyekukosea.
Hebu fikiri ungenyamaza ungeangamiza wangapi? Maana kuna ukweli ulikuwa nao moyoni mwako. Na unajua kabisa hatari iliyopo kwa rafiki yako wa karibu ni kubwa.
Kuinua sauti yako kusema juu ya kile unaona kingemwangamiza yule mtu asingeambiwa, utakuwa umefanya jambo la maana sana katika maisha yako.
Hapo utakuwa umeona kunyamaza kulivyo na pande mbili na zote zina maana yake, sio nyakati zote kunyamaza inafaa. Na sio nyakati zote kutonyamaza inafaa, elewa hilo.
Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com