Ulivyokuwa nyuma inaweza isifanane kabisa na sasa ulivyo, inawezakana kabisa ulivyokuwa nyuma ni afadhali kuliko sasa.

Inawezekana ulivyo sasa ni hatua kubwa sana kuliko ulivyokuwa huko nyuma, na inawezakana ulipo sasa umeshuka sana kuliko huko nyuma.

Inawezekana kiwango chako cha ukuaji kiroho kimeongezeka sana kuliko huko nyuma, na inawezekana kiwango chako cha kiroho kimeshuka sana kuliko huko nyuma.

Inawezekana mtaji wako mdogo ulioanza nao biashara huko nyuma umekua sana, na sasa unaongelea mamilioni ya fedha. Na inawezekana mtaji wako mkubwa wa biashara uliokuwa nao huko nyuma umeporomoka sana.

Inawezekana bidii yako ya ibada huko nyuma ilikuwa ndogo sana ukiilinganisha na sasa, ama inawezekana huko nyuma ulikuwa na bidii kubwa sana na sasa hiyo bidii haipo tena.

Nimejaribu kukutolea mifano kadhaa vile ulikuwa nyuma na sasa ulivyo, unaweza kuongeza mifano mingine zaidi kadri unavyozidi kutafakari.

Hebu fikiri ulipo sasa na huko nyuma kipi kimeongezeka kwako, na kipi kimepungua kwako. Jaribu kufikiri, inawezakana unajidanganya upo vizuri  ila kumbe una hali mbaya.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com
+255759808081