Kuna kitu kinaweza kikatokea ukaambiwa maneno fulani ya kukuumiza moyo wako.

Wanaweza wakawa wanasema kweli au wanaweza wakawa wanaongea maneno ya uongo.

Anaweza akatokea mtu akakuambia maneno ambayo kwako yakawa na maswali mengi au yakazua sintofahamu kwako.

Ninachotaka ukielewe hapa na ufikiri zaidi ni kwamba kwanini wakuambia hayo waliyokuambia.

Uwe umefurahi, ama uwe hujafurahi, kipi kimewafanya wakuambie hivyo, ukifikiri vizuri utajua ni kwanini wamekuambia.

Kama wamekuambia maneno ya kukuvunja moyo jua ya kwamba ipo sababu iliyowasukuma wakuambie hivyo.

Kama wamekuambia hutokaa uweze ipo sababu ambayo imewafanya wapate nguvu ya kukuambia hivyo.

Mtu hawezi kutoka huko atokako akaja kusema maneno mabaya juu yako, au akaja akasema maneno ya kukutia moyo.

Lipo kusudi la Mungu wakati mwingine uambiwe hayo uliyoambiwa, unaweza usielewe sana wakati huo ila baadaye utakuja kugundua haikuwa hivi hivi.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest.
www.chapeotz.com