Sifikiri kama kuna mtu anaweza kufanya kitu bila kutegemea kupata faida, hata mtu anayeua wengine atakuwa anategemea kupata kitu fulani baada ya kufanya hivyo.

Ikiwa mtu anafanya kitu au jambo kwa kutegemea faida, au kutegemea kupata matokeo fulani mazuri kwa manufaa yake, au kwa manufaa ya wazazi wake, au kwa manufaa ya watoto wake, au kwa manufaa ya taifa, au kwa ajili ya kumletea Mungu utukufu.

Hata katika maisha yetu kuna vitu tunapaswa kuvifikiri vizuri, maana yapo mambo tunakuwa tunayafanya, au tunakuwa tunayashikilia mioyoni mwetu. Alafu mwisho wake yanatufanya tuingie hasara wenyewe, tena hasara kubwa.

Hebu fikiri kuna mtu amekukosea jambo fulani, tena jambo lenyewe ni zito haswa, na umeshasema huwezi kumsamehe. Umewahi kufikiri ipi faida unayoipata kwa kufanya hivyo?

Usipomwachilia moyoni mwako, ukaendelea na msimamo wako wa kutomsamehe kamwe, ipi faida unayoipata kwa kufanya hivyo?

Ukifikiri vizuri utaona hakuna faida ya kuendelea kumshikilia mtu moyoni mwako, hata kama hajaja kukuomba msamaha. Hata kama hajaonyesha kuwa amekukosea sana, maana tayari umeshaona haina haja ya kuendelea kumshikilia mkosaji moyoni mwako.

Maana kama amekutendea jambo lisilofaa na hajachukua hatua yeyote ya kukuomba msamaha, ama hajachukua hatua yeyote kwenda mbele za Mungu kutubu. Hicho kisasi kitakuwa ni cha Bwana mwenyewe, wala wewe hupaswi kujua atamfanyaje.

Uache kujitesa na mambo unayoyarundika kwenye moyo wako, huku umeweka msimamo wa kutoachilia. Kufanya hivyo hakuna faida yeyote unayoipata kwenye maisha yako.

Mungu akubariki sana.
Ndugu yako katika Kristo,
Samson Ernest,
www.chapeotz.com
+255759808081